Thursday, September 8, 2016

Maana ya alama zilizopo kwenye miili yetu.

Kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa uwepo kwa baadhi ya alama kwenye miili yao huwa na maana kwenye maisha yao.Inaweza kuwa bahati,nuksi  au pengine huwakilisha tabia ya tofauti kwenye mwili wa mtu husika.

Hizi ni baadhi tu ya maana ya alama hizo,ila ikumbukwe kuwa alama hizi ni zile za kuzaliwa na sio makovu.

ALAMA NA MAANA ZAKE.

Mguuni,mkononi au kwenye vidole -Kwa wachina alama kwenye mwili inawaweza kuwa bahati au nuksi ila inategemea ina rangi gani na ipo sehemu gani,kwa mfano alama yenye rangi nyeusi ikiwa mguuni inaelezea mhusika ni mtu wa kusafiri,inaweza pia kuwa alama yenye rangi ya "dark red" rangi ya damu ya mzee kama wengi wanavyoiita na ikiwa ipo mkononi humanisha kuwa mhusika ana ujuzi fulani au jambo fulani linalohusu mkono huo.
                                    Mwanamuziki Vanessa Mdee.

 Karibu na Pua -Inadawa alama inapokuwa kwenye eneo la uso humaanisha mambo mazuri ila inategemea alama ipo eneo gani,watu hawa wengi huwa maarufu,wenye ujuzi wa tofauti ila pia ikiwa karibu na pua humanisha mhusika sio mtu wa kukasirika mapema.Pia baadhi yao huwa na sifa ya kuwa viongozi.
                         Jaji na waziri mkuu mstaafu,Joseph Sinde Warioba.

Mdomoni - hapa humanisha mhusika kuwa na maisha ya wastani,mafanikio,umaarufu ila pia kwa upande wa wanaume humaanisha mhusika ni mtu wa kupenda wanawake.

                                             Mwigizaji Angelina Jolie.

Kichwani - Hapa humaanisha mhusika amejaliwa madaraka katika mambo fulani,wengi wao huwa wanasiasa au wanaharakati.Pia hupenda mijadala na kujishuhulisha hata kwenye mambo yasiyowahusu.

Kwenye jicho kulia au kushoto - Humaanisha mhusika kuwa mtu wa bahati na fedha,anaweza asiwe mtafutaji ila ni mtu mwenye bahati.Kwa upande wa wanaume alama ikiwa pembezoni mwa jicho humaanisha mhusika ni mtu wa kupenda wanawake na ni msiri sana,jambo linalomuhusu hawezi kuongea mbele za watu,mara nyingi huwa kimya na  hawapendi kuzungumza maana muda mwingi wanautumia kuwaza mambo yao.Ila sio watu wenye kupenda ugomvi lakini  pia alama ikiwa chini ya jicho humanisha upendo au upole.

                                   Mwanamitindo,Jokate Mwongelo.

Kwenye sikio,shingoni au nyuma ya kichwa - Hapa humaanisha mhusika ni mtu wa kujiheshimu na mwenye  mipango,huwezi kumdanganya kirahisi kwa kuwa hufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi.

                                        Rapper na mfanyabiashara,P-Diddy.

Kwenye ulimi - Hapa humanisha mhusika kuwa tatizo la kiafya japo linaweza lisionekane mapema,wengi wao huwa wazungumzaji na wenye umakini sana.Pia wanapenda kula,kucheza na kuongea na watoto ila pia ni watu wenye maono.

                                           Raisi Barack Obama.
  
Kwenye bega au mgongoni - Hapa humanisha mhusika kuwa mtu wa kupenda marafiki,ni watu wenye hisia na ni rahisi kuwa rafiki wa mtu yeyote.

                                               Rapper,Nas Escobar.

 Puani - Ni maajabu ila inadaiwa alama inapokua puani humanisha nukisi au jambo baya kwenye maisha ya mhusika.Mara nyingi ni watu wa kupenda starehe,wenye hasira ila pia huandamwa na changamoto nyingi kwenye maisha yao.
Je unafikiri mitazamo hii ina ukweli ndani yake...??









     

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.