Kaka yetu
ndugu yetu wa damu Rapper Chidi Benz weekend hii alimalizia pasaka yake akiwa selo ya polisi, na anashikiliwa
kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi vibaya mwanamke anayeitwa mwanaisha ktk bar
moja iliyopo maeneo ya flat za ilala boma, amefunguliwa kesi iliyopewa rb
ilala/1569/2014
Mwanaisha
amepasuka mdomo na kushonwa minyuzi 18, hawezi kuongea uso umeumuka, bichwa
limevimba,
Halafu
mwanaisha inaonekana mambo ya nyoshi yale kitaulo kwa mbaaali, kwa hiyo ngozi
ya kchwa imekua nyekunduuuuuuuuuu, Chidi benz nae ana jeraha kichwani
Kwa mujibu
wa Chidi Benz amedai kuwa eti huyo mwanaisha aliwahi kuwa mpenzi wake miaka ya nyuma, na inavyoonekana mwanaisha ndiye alimpigaga kibuti chidi benzi
inasemekana lakini
Sasa usiku
ya tukio, siku ya pasaka Chidi anasema alikua anarudi kwake Maeneo ya Ilala
Boma Flat akiwa ameongozana na dem wake wa sasa hivi mpyaaa
Pembeni pale
chini kwao kuna bar
Mwanaisha
akamwita Chidi naona uko na mama watoto
We chidi
benzi naona uko na mama watoto kama mara tatu au nne
Sasa
kilichofata baada ya hapo Chidi akawa anaskilizia nani anayemwita gizani ndo
akasogelea eneo alikuwepo mwanaisha na wenzake kama nane au zaidi, na kumwambia
mbona unanichora au kwasababu niko na demu mkali kuliko wewe unaona wivu, Chidi
anasema eti Mwanaisha akamrushia chupa ya Kichwa na kumpasua damu zikaanza kumwagika,
ndo yeye anachokumbuka alimshika nywele tu mwanaisha kilichofata baada ya hapo
hakumbuki kwasababu alikua amelewa.
Mwanaisha
akapanda taxi vuuuup
Huku nyuma
watu wakamshtua chidi oya, mwenzio anawahi polisi
aaaah chidi naye mbio mbio akakimbilia na yeye
kwenda kushtaki
Mwanaisha
kishafika kituo cha polisi pangani ilala, polisi kumwona chidi eheeee umejireta
mwenyewe
Patamu
Akavuliwa
mkanda, akaandikisha vitu alivyokua navyo,
kile kihereni anachovaaga puani nacho akavuliwa, vuuup ndani
Mi jana
nikaenda pangani kituo cha polisi nikamwona ndugu yangu, tukaongea mengi lakini
kwa sababu kesi iko mahakamani sidhani kama ninaruhusiwa kuyazungumza hapa.
Leo asubuhi
ngoma mahakama ya mwanzo ilala, mwanadada mwanaisha ameshindwa kuongea lolote
mahakamani kutokana na maumivu yanayotokana na mshono wa mdomoni, nyuzi 18
mchezo sasa cjui nani kampiga
So akaambiwa
aende hospitali, manake unaambiwa mwanaisha anazimia zimia kila wakati
Na kwa
mujibu wa wataalamu wa mambo, chidi hawezi kupewa dhamana mpaka mwanaisha arudi
sawa kidogo manake lolote linaweza kutokea hatuombei apoteze maisha.