Thursday, May 9, 2013

VIDEO : POLISI AKUTWA NA KICHWA CHA BINADAMU ALICHOKUA ANATAKA KUMSAKIZIA MFANYABIASHARA

                               


WATU wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro akiwemo askari polisi watatu wa jeshi la polisi mkoani Morogoro na raia mmoja  kwa  kuhusishwa na tuhuma za kumbambikizia tuhuma za kukutwa na kichwa cha binadamu mfanyabiashara wa mjini Dumila wilayani Kilosa mkoani hapa.

Wakizungumza na Clouds Tv  wananchi wa mtaa wa Mgudeni Dumila wilayani Kilosa akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo Zaituni  Kifutu,MOhamed Fungafunga na Musa Magisu wanasema tukio hilo ni la kushangaza ambalo limetokea leo na kwamba polisi kwa kushirikiana na raina mmoja wanadaiwa kubambikizia tukio hilo mfanyabiashara wa eneo hilo Samson Mura ambapo walimtaka kutoa shilingi milioni ishirini na tano ili waweze kumwachia kitendo ambacho alikipinga.

kwa upande wake afisa upelelezi msaidizi wa polisi mkoa wa Morogoro Asifiwe Ulime  amekiri  kutokea tukio hilo na alifika eneo la tukio na kushuhudia fuvu hilo ambapo alisema kuwa askari hao watatu akiwemo na mwananchi huyo mmoja wanashikiliwa na jeshi la polisi ili watoe maelelezo ya kina na kuwaomba wananchi wa Dumila kuwa watiulivu wakati uchunguzi unaendelea.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.