Tuesday, April 22, 2014

MAJERAHA YA AJALI BADO YAENDELEA KUMTESA PRODUCER C9

C9
Ajali ya Bajaj aliyopata Producer C9 Kanjenje imemsababishia maumivu ya macho na jeraha kubwa kichwani, Ajali hiyo ilitokea jumamosi ya Pasaka Usiku mida ya Saa nne maeneo ya Leaders Club Kinondoni, baada ya bajaj aliyokua amepanda Producer huyo na rafiki zake kugongwa na gari kwa nyuma, usiku huo huo C9 aliwahishwa hospitali kwa matibabu lakini kesho anatarajia kurudi hospitali kwa ajili ya kufanya vipimo zaidi ili kujua ndani ya kichwa chake kuna uharibifu wa kiasi gani, C9 anasema kwa sasa hivi hawezi kufanya kazi zake za utaarishaji wa muziki kwa sababu kila hawezi kuangalia computer macho yanamuuma na akisikiliza muziki pia kichwa kinamuuma.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.