Monday, August 11, 2014

NDOA YA LADY JAY DEE NA GARDNER G HABASH YAVUNJIKA

Ndoa kati ya Msanii wa Bongo Flava Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee na Gardner G Habash inasemekana kuwa imevunjika na inasemekana eti tayari Bwana Gardner ameondoka katika nyumba aliyokua anaishi na mke wake maeneo ya kimara na kuhamia kwa moja kati ya ndugu zake.
Chanzo cha ndoa hii kuvunjika bado hakijajulikana, tunaendelea kufatilia, ila habari kutoka kwa watu wa karibu na familia hii zinadai kuwa hii si mara ya kwanza kwa Lady Jay Dee kutengana na Gardner ila safari hii wanashindwa kutabiri kama watarudiana au ndo kutemana milele, ila fahamu tu kwamba si ngumu sana kuvunjika kwa Ndoa hii kwa sababu hawaku oana kanisani kwa sababu tayari G alishaoa kanisani na kupata mtoto mmoja, wakahofia mama wa mtoto huyo angeweka pingamizi kupinga ndoa hiyo isifungwe.
Gadner G Habash na Judith Wambura walifunga ndoa kabambe ambayo ili make headline zaidi ya miaka tisa iliyopita, na kuhudhuriwa na Mastar kedekede.
Inaonekana huu ni mwaka wa shetani kwani hii si ndoa ya kwanza ya watu maarufu kuvunjika, tayari ndoa ya Dida wa Mchops na Ezden Jumanne imevunjika na wawili kurushiana madongo, na kuna ndoa nyingine tia maji tia maji ngoja yakamilike nitakufahamisha.
Pyaaaaaaaaaaaaa.........

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.