Thursday, September 8, 2016

Hatimae binti aliekua akiandika kwa kutumia ulimi apata kifaa cha kuandikia.



Unamkumbuka Wakonta Kapunda yule Binti Mtanzania mwandishi wa miswada ya filamu aliekua akiandika  kwa kutumia ulimi wake baada ya kupooza.

Wakonta alipata ajali siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita. Ajali hiyo ilimuacha akiwa amepooza kwanzia shingoni kushuka chini na kumfanya kutoweza kutumia mkono yake kuandika ambapo kupitia kipindi cha televisheni cha Focus on Africa katika BBC World Service, mwanadada Olivia Soko kutoka  nchini Afrika ya Kusini aliguswa na kuamua kumsaidia Wakonta kwa kumpa  kifaa maalum kitakachomsaidia kuandika.

                                              Wakonta akitumia kifaa hicho.

 Jinsi Program hii inavyofanya kazi ni kwamba mtumiaji yeye anazungumza anachotaka kukiandika kupitia kipaza sauti chake halafu programu hii inaandika yenyewe katika kompyuta ya mtumiaji.

 Akiwa mkurugenzi wa kampuni ya Whirlmarket Technologies, Olivia (kulia) alietoa msaada wa kompyuta inayotumia programu ya kompyuta iitwayo Nuance Dragon Naturally Speaking.

 Chanzo:BBC Swahili

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.