Jumatano hii muimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha inayoonesha muonekano wake mpya tangu aliposaidiwa na polisi mapema mwaka huu baada ya kuzidiwa na matumizi ya madawa kulevya kiasi cha kutishia kujiua.
Hata hivyo picha hiyo imewafanya mashabiki kumtaka kuachana na matumizi ya
Madawa ya kulevya kwa kuwa amekuwa akisaidiwa mara kadhaa kuachana na
matumizi ya Madawa ya kulevya lakini yeye amekuwa akirudia ambapo kwa sasa yupo kwenye kituo cha matibabu kwa waathirika wa madawa hayo cha Pili Masana,Kigamboni jijini Dar es salam.