Kwa mujibu wa mashuhuda,watu 4 wamejeruhiwa baada ya gari moja katika msafara wa Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan kupata ajali na kupinduka eneo la Nanguruwe wakati msafara
huo ukitokea mkoani Mtwara kuelekea Tandahimba ambapo majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula.
Makamu wa Rais yupo mkoani Mtwara katika ziara ya kikazi ya siku nne
ambapo pamoja na mambo mengine amefungua ofisi ya
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini hafla
iliyofanyika mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan.
Tutaendeleea kufatilia taarifa hizi kwa undani na kuwahabarisha.