Tofauti na watu wengi walivyotarajia,video fupi iliyosambaa mtandaooni imewaonesha wapenzi hao wa zamani wakikumbatiana wakiwa kwenye bus la wasanii hali iliyoamsha shwangwe miongoni mwa wasani wenzao.
Nuh Mziwanda anatamba na hit's yake ya "Jike Shupa" ambayo inadaiwa amemuimbia Shilole mara baada ya mapenzi yao kufika tamati wakati Shilole akisumbua na hit's yake ya "Mtoto Mdogo" ambayo mashairi yake yameakisi mahusiano yake na watu aliowazidi umri akiwemo Nuh Mziwanda.
Swali la kujiuliza je wawili hawa watapanda jukwaani pamoja hasa ikizingatiwa kuwa Tabora ndio mkoa anaotoka Shilole.Nadhani mashabiki wa Mkoa huu wata-enjoy kitu cha tofauti zaidi.