Wednesday, September 7, 2016

VIDEO:"Nas Album Done",Dj Khalid na Nas wamethibitisha.


Wakati ambao album yake ya "Major Key"ikiendelea kusumbua kwenye chati kubwa za muziki duniani,Dj Khalid ameungana na rapper mwenye heshima katika muziki wa Hip Hop ulimwenguni Nas Escobar na ku-share kionjo cha video fupi kilichorekodiwa kwenye mitaa ya jiji la Bahama huku video hiyo ikiashiria kuwa colabo yake na Queen's Bridge rapper,Nas Escobar katika wimbo wa "Nas Album Done" unaopatikana kwenye album yake ya "Major Key" imekamilika.
Hata hivyo hii ni mara ya pili kwa Dj Khalid kupost video inayomzungumzia Nas kwani mwezi October mwaka huu alipost video nyingine na kuandika.... "I prayed for times like this,” ..... “I remember having @nas illmatic poster hung up in my garage with my two turntables and drum machine!! Look at me I’m with @nas."



 Khalid amekua na bahati kwenye muziki wa Hip Hop kwani licha ya album yake ya "Major Key" kupata mafanikio makubwa ikiwajumuisha wakali wengi wa muziki huo nchini Marekani,pia atazisherehesha tuzo za BET-Hip Hop Awards zinazotarajiwa kutolewa September 17,mwaka huu.





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.