Kwa mujibu wa dada wa mwanariadha huyo,Christine Bolt-Hylton (32) amedai kuwa wawili hao kwa sasa wamemaliza tofauti zao na wanaonekana kupendana zaidi.."I'm sure Kasi will be used to it by now....."She is used to seeing pictures like this".."People ask for pictures with him and he is always willing to have pictures".. "She is used to him being in the public domain."
Hata hivyo tetesi za Bolt kumvisha Bennet pete ya uchumba zimekuja mara baada ya wawili hao kuingia kwenye mgogoro baada ya picha za faragha za mwanariadha akiwa na binti mwanafunzi raia wa Braazil Jady Duarte (20) kusambaa kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini Rio nchini Brazil.
Picha iliyosambaa kupitia mtandao wa whatsaap na kuleta mtafaruku kwenye mahusiano ya wawili hawa.
Mpaka sasa Usain Bolt ndie binadamu mwenye kasi zaidi ulimwenguni,huku akiweka na kuzivunja rekodi zake mwenye ambapo katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika nchini Brazil mwaka huu amekua Mwanariadha wa kwanza kuweka rekodi ya kushinda medal tatu za dhahabu,mita 100,mita 200 na mita 100 reley.