Mnamo tarehe 14 Disemba mchana Polisi kutoka kituo cha Kati, Dar es salaam
wakiambatana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Jamii Media,inayomiliki mtandao wa 'Jamii Forum' Ndugu Maxence Melo,
walifika katika ofisi za Jamii Media kwa ajili ya ukaguzi.
Zoezi hilo lilienda sambamba na kuwahoji wafanyakazi (Social Media
Engagers na Content Quality Controllers) juu ya utendaji wa shughuli zao
za kila siku ndani ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam na kuondoka na wafanyakazi wawili kwa mahojiano zaidi ambapo walielekea nyumbani kwa Maxence Melo kwa ajili ya ukaguzi ndani ya nyumba.
Katika zoezi zima la ukaguzi, sehemu zote
mbili, Jeshi la Polisi halikuhitaji wala kuchukua kifaa cha mawasiliano
ya kimtandao kama router, flash, hard disc, au kompyuta ila walichukua baadhi ya nyaraka za usajili wa kampuni hiyo.
Eneo la nnje la nyumba ya Maxence Melo.
Hata hivyo baada ya ukaguzi huo kwenye nyumba ya Bwn.Melo,msafara huo ulielekea kituo cha kati kukamilisha mahojiano kati ya Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wawili waliochukuliwa.
Credit:Mashuhuda wa SHILAWADU.