Showing posts with label Manchester United. Show all posts
Showing posts with label Manchester United. Show all posts

Thursday, October 13, 2016

PICHA:Watoto 2 wa Zalatan Ibrahimovic wajiunga na timu ya watoto ya Man-United baada ya timu hiyo kumsaini mtoto wa Wayne Rooney mwenye umri wa miaka 6.


Wakati sakata la Mshabuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza kuhusu kiwango chake na ushiriki wake kwenye timu ya taifa  likiendelea kutokota,Klabu ya Manchester United imemjumuisha mtoto mkubwa wa Mshambuliaji huyo  kwenye 'Academy' ya timu ya watoto ya klabu hiyo ambapo amekua akifanya mazoezi na timu ya watoto ya klabu hiyo.

Mtoto wa Wayne Rooney,Kai.


Kai Wayne Rooney mwenye umri wa miaka sita ataungana na watoto wa Mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic ambae nae amewapeleka watoto wake wawili,Max (10) na Vincent (8) ambapo pia watajumika na watoto wa wakongwe wengine kama Michel Carrick,Ryn Giggs na Nick Butt ambao nao watoto wao wamejumuishwa kwenye timu hiyo ya watoto ya klabu hiyo.

Wayne Rooney na watoto wake,kwenye moja ya michezo ya Manchester United.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun,klabu hiyo imepanga kukuza vipaji vya watoto wa mastaa hao walioitumikia klabu hiyo kama sehemu ya kuenzi mchango wao na sifa waliyoipatia klabu hiyo.

  "The hope at the club is some of their dad’s talent has rubbed off on the youngsters"..."Manchester United is  known for its  youth development, and this is just another stride towards finding stars of the future,United have some of the best youth coaches in the world, and the players know they’re in the right place".Sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Monday, September 19, 2016

Baada ya Man-United kukubali kichapo,Madee ajibu post ya Pogba Instagram.

Klabu ya Manchester United  kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha juma moja imepoteza michezo yake tena ikikubali kufungwa na klabu ya Watford kwa magoli 3-1.

Watford walikuwa wa kwanza kupata goli lilifungwa na Daryl Janmaat kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.Ila kiungo wa Watford Zuniga alifunga ikiwa imesalia dakika saba mchezo kukamilika kabla ya Deeney  alifunga penalti katika muda wa ziada baada ya Marouane Fellaini kumchezea vibaya katika eneo la hatari.

Hii ni mara ya tatu mfulilozi kwa Manchester United kupoteza,ikishindwa 2-1 na Manchester City,baadaye ikapoteza 1-0 dhidi ya klabu ya feyenoord ya Uholanzi katikati ya wiki katika kombe la bara Ulaya.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Mshambuaji wa Manchester United,Paul Pogba ali-post ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwashukuru mashabiki wa United na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito hali ilipelekea mashabiki wengi kuponda ujumbe wa mshambuliaji huyo aliesajiliwa kwa kiasi cha $105m.

Miongoni mwa walitupa madongo kwa mshambuliaji huyo ni Mwanamuziki wa Bongo fleva,Madee Ali  ambae ni shabiki wa Unite alie-coment kwa kuandika "U can wapi ww rudisha mapene ya watu..ww mtu gani ufungi..mbona xhaka kafunga jana".Aliandika Madee.


 Swali la kujiuliza,kwa lugha aliyotumia Madee ujumbe utakua umefika kweli...!!!.


Sunday, September 11, 2016

VIDEO:Jose Mourinho awatupia lawama mastaa wake.

Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake  akidai  kuwa wao  ndiyo sababu ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya mahasimu wao Manchester City kwa mabao 2-1.

                                                     Jose Mourinho.

Man United walijikuta wakipotezwa kabisa na vijana hao wa Pep Guardiola kwenye dimba lao la Old Trafford, na kujikuta wakiruhusu magoli mawili yaliyofungwa na Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.

 Baada ya mchezo huo Mourinho alisema: "Wakati mwingine wachezaji huwavunja moyo mameneja wao".Alimwambia ripota wa Sky Sports.  “Kipindi cha kwanza walikuwa vizuri zaidi yetu"....."Tulianza mchezo huku baadhi ya wachezaji wakicheza chini ya kiwango chao cha kawaida kuanzia kwenye suala la umakini mpaka kasi ya mchezo".

              Jose Mourinho (L) na Meneja wa Man-City,Pep Guardiola wakati wa mchezo.

"Unahitaji kuwa na maamuzi ya haraka namna unavyocheza na unavyofikiri"..."Mchezaji mmoja au wawili hivi walikuwa hawapo kwenye kiwango kizuri na hali hiyo imeigharimu timu".Aliongeza Kocha huyo mwenye tambo nyingi.

Mourinho aliwaanzisha Jesse Lingard na Henrikh Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza lakini aliwatoa wote baada ya kipindi cha kwanza kuisha baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.