Tuesday, March 11, 2014

BABU AYUBU KATIKA BEEF KUBWA

,
Mkali wa kuigiza sauti za watu maarufu Babu Ayubu hivi karibuni amedondosha ngoma "Shikamoo Pesa" aliyoigiza sauti za wasanii Crazy GK, Bi Kidude, Mheshimiwa Temba, Nay wa Mitego, Chidi Benzi, Inspektah Haroun na Sugu, ukisikiliza Ngoma hii juu juu utaishia kucheka kutokana na na kipaji cha msanii babu kuigiza sauti za wasanii hao wote kwa umahiri, lakini zaidi ya yote Babu Ayubu amezungumzia jinsi pesa inavyoweza kujenga uadui na Urafiki, MC Babu Ayubu amesema Chanzo cha Beef iliyowahi kutokea kati ya Mwana Fa na Ambwene Yesaya dhidi ya Gk eti ilisababishwa na Pesa, na eti Gardner na Jay Dee eti hawapatani na best man wao Mwana Fa kwasababu ya Pesa, Babu Ayubu amesema Pesa ilileta Beef Kati TMK Halisi na TMK wanaume hapo ametumia Sauti ya GK kuelezea hayo,Sauti ya Mheshimiwa Temba amezungumzia eti Wasanii wanatumika kwenye biashara ya Madawa ya Kulevya na mchongo ukibuma wanatia Huruma,
Sauti ya Nay wa Mitego imempiga dongo Babu Ayubu kwa kumwambia Njaa haina Baunsa ndio maana Babu Ayubu amewahi kuimba Taarabu, Kingereza Kingi bila pesa hayo ni makele, halafu eti kama huna hela na una Upara Kichwani basi hilo ni Kovu,
Sauti ya Sugu imeanza kwa kuwataja Wakurugenzi Tale na TipTop, Fela na T.M.K mara wasanii wao tu ni wadogo wadogo ila kiutani wana mijumba na Migari Town, kuliko ...........walim manage Man - Dojo na DomoKaya wakafanya show mpaka Ulaya, bila haya mwisho wa mchezo wakaachwa na hali mbaya bila hata pa kulala yote sababu ya Money watu walipewa Pesa wakamhujumu Lowasa akaona isiwe tabu akabwaga mpaka sasa, Mwendo wa Pesa Zito Kabwe kaamua kutuuza (Hapa atakua kazungumzia sakata la Zitto Kabwe na Chama Chake cha Chadema, baada ya kutuhumiwa kukihujumu)
Kiitikia kina Sema "Shikamoo Pesa mi Nasema Shikamoo Money" Mar'habaaaaa
Sikiliza Ngoma Hiyo hapo chini:

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.