|
Cosmas Chidumule |
Muimbaji Veteran katika Tasnia ya Muziki, ambaye alianzia kwenye Muziki wa Dansi na baadae kuokoka na kuanza kufanya vizury muziki wa Gospel Mzee Cosmas Chidumule amejikuta anadumbukia mzima mzima kwenye Kashfa ya utapeli, baada ya Kampuni moja iliyopo Njombe kudai kuwa mwaka 2010 waliingia mkataba na msanii huyo, kwa kununua hakimiliki ya baadhi ya nyimbo zake za Audio ili kampuni hiyo izifanyie Video na kuziuza, biashara nzima ilikua na thamani ya milioni kumi, wao wakampatia mzee huyo milioni sita lakini tangu siku hiyo mzee huyo hajaonekana Location kwa ajili ya kushoot Video hizo na ilipofika mwaka 2013 mwezi wa Tisa wakaamua wakafungue kesi mahakamani, hiyo ni baada ya chama cha hati miliki Tanzania (COSOTA) kushindwa kutatua mgogoro huo kutokana na Mzee Chidumule Kushindwa kufika kwenye vikao vya usuluhishi, akizungumzia Sakata hilo Mzee Chidumule amekanusha shutuma hizo na kudai kuwa hiyo ni kazi ya shetani, akiwa na maana kuwa hawezi kupiga tukio kama hilo ukizingatia yeye ni mtumishi wa mungu, so mpaka sasa hivi Kesi iko mahakamani pande za Njombe.....kwa info zaidi ntakufahamisha kupitia Gazeti pendwa la Makorokocho......