Kundi la muziki wa Bongo Flava Off Side lililokua linaundwa na wasanii wawili Lil Gheto na Hammer Q limemeguka kwa mara ya pili, Mara ya kwanza Msanii Mudathir Masoud (Mudachris) alijitoa kwenye kundi hilo na kuachana na muziki kwa sababu aliamua kubadilisha njia kwa kujikita zaidi na ibada za dini ya kiislamu ndipo Msanii aliyebaki Lil Gheto akamshawishi Solo Artist Hammer Q ajiunge kwenye kundi hili ili kuongeza nguvu, sasa ikiwa haijatimia hata miaka miwili Hammer Q nae amenyoosha mikono juu na kuivua kofia ya Offside Trick kutokana na kutoridhishwa na Mgawanyo wa pesa inayotengenezwa na wao wawili, habari za chini chini zinadai kuwa eti Lil Gheto alikua hataki kwenda kuperform kwenye Shows alizokua anatafuta Hammer Q lakini show akiipata yeye Lil Gheto walikua wanaenda wote kutumbuiza ila kwenye kipato eti Hammer Q alikua hapewi anachostahili, sababu nyingine inayosemekana kumkimbiza Hammer Q eti ni kwasababu Lil Gheto hayuko serious kwenye ku promote nyimbo za kundi kwasababu ana studio "Akhenato" inayomwingizia Pesa hivyo hata kundi lisipoingiza pesa yeye hajali hali ambayo inamuumiza Hammer Q kwasababu yeye kajitolea muda wake wote kulitumikia kundi.
Sasa wakati akijibu shutuma hizi Lil Gheto amesema wiki moja iliyopita alipokea ujumbe mfupi wa maneno kwa njia simu kutoka kwa Hammer Q ukidai kuwa ameamua kufanya kazi zake binafasi, na akadai kuwa Hammer Q alikua anatafuta show kweli lakini zilikua ni za kurisk kwasababu walitakiwa kuperform kwanza kisha ndo walipwe kutokana na maingizo hali ambayo yeye Lil Gheto hakubaliani nayo kwani anabiashara zake ambazo zinahitaji usimamizi so bora kulipwa kwanza kisha ndo wapige show.