Baada kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na silaha pamoja na kusafirisha madawa ya kulevya mwishoni mwa wiki iliyopita,Hatimae rapper Disigner amefutiwa kosa la kukutwa na silaha kinyume na kibali baada ya uchunguzi kubainisha kuwa rapper huyo hakua na silaha kwenya gari wakati anakamatwa ila bado ana kesi ya kujibu juu ya tuhuma za kukutwa na aina tofauti za madawa ya kulevya kama OxyContin, methadone na steroids.
Mara baada kuhojiwa na na Polisi na kisha kufutiwa kosa hilo,hit maker wa single ya "Panda" ambae yupo chini ya music label ya GOOD MUSIC inayomilikiwa na rapper Kanye West amepost video kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuelezea kilichomkuta. “Ni**as is crazy,” .......“We back out here, man. You dig? Ni**as crazy. I heard ni**as say we had to sell pills? We don’t gotta do that shit no more, baby. We don’t do this no more, baby…Out here, man. Back in the city” .Anasikika Disiigner kwenye video hiyo.
Inadaiwa kuwa mnamo Sept.9 rapper huyo akiwa kwenye gari na marafiki zake wanne wakitoka kuhudhuria onesho la mavazi ya bosi wake "Yeezy Season 4" Jijini la New York alijibizana na mtu dereva wa gari jingine hali iliyopelekea mtu huyo kuwapigia simu maafisa wa Polisi huku akiidai kuwa rapper huyo alimtishia na silaha.