Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts
Saturday, December 17, 2016
Ujerumani kuzipiga faini Facebook,Twitter na Google kama hawatazivuta Habari za Kichochezi.
Serikali ya Ujerumani kupitia waziri wa Sheria Heiko Maas inatarajia kuwawekea vikwazo ikiwepo FAINI makampuni makubwa ya Mitandaoni Facebook,twitter na GOOGLE kama hawatafuta Hotuba za Chuki kwenye mitandao yao.
Serikali hiyo imewapa hadi masaa 24 yajayo wasipofuta habari hizo za chuki watapigwa fine isiyopunga TSH 1 Billion. Tayari kikosi maalumu cha facebook,twitter na GOOGLE kilikaa mwaka jana kushughulikia tatizo hilo lakini ripoti kutoka serikali ya Ujerumani inadai kuwa taarifa hizo nyingi hazijachukuliwa.
Heiko Maas,Waziri wa Sheria Ujerumani.
Tayari kwa Upande wa Facebook Hivi juzi wamezindua SOFTWARE maalum ya kugundua Taarifa Feki katika mtandao wake kabla haijarushwa.
Miongoni mwa taarifa zinazotajwa kuwa chanzo cha sakata hilo ni taarifa za kichochezi juu ya hatua ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya na taarifa za uzushi juu kauli za viongozi wa Umoja huo juu ya ushindi wa Donald Trump kuwa rais wa Marekani,ushindi ambao uliwashangaza wengi ulimwenguni hasa kutokana na misimamo na kauli zake tata wakati wa kampeni.
Unaweza kusoma habari nzima kwa kubofya link hapa chini.
Germany to force Facebook, Google and Twitter to act on hate speech
Friday, December 16, 2016
Hizi ndizo sababu za Kafulila kuhama NCCR-Mageuzi na kuhamia Chadema.
Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) David Kafulila,amekihama chama hicho huku na kueleza kuwa anajiandaa kuhamia CHADEMA.
Mbunge huyo machachari anakumbukwa kwenye historia ya siasa za Tanzania hasa pale alipoibua bungeni sakata la ufisadi wa akaunti ya Escrow mnamo mwaka 2015.
Chanzo:Mwananchi.
Mkurugenzi Jamii Forum afikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka matatu.
DAR ES SALAAM-Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Melo mapema leo amefikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa mashtaka matatu likiwemo shitaka lakuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao. kati ya mashtaka hayo,mawili amepata dhamana huku la tatu likiendelea kuwa kizungumkuti cha Bwan.Melo kukosa dhamana.
Mawakili wanaomtetea wanaendelea kushughulikia dhamana ya mteja wao ambae tayari anaidaiwa amepelekwa gereza Keko.
HIZI NI HATI ZA MASHTAKA
Kwa siku tatu mfululizo Jeshi la Polisi lilimshikilia Melo ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media inayomiliki mtandao wa 'Jamii Forum',akitakiwa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
Serikali yasitisha ajira za Walimu wa masomo ya Sanaa.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako, ametoa masharti mapya ya ajira za ualimu nchini, huku
akisema Serikali haitaajiri walimu wa masomo ya sanaa (arts) kwa kuwa
wapo wa kutosha.
Akizungumza mjini Dodoma jana wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Profesa Ndalichako, alisema Serikali kwa sasa haiwezi kuajiri walimu wa masomo hayo kwa kuwa inataka kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ambao idadi yao ni ndogo.
Pamoja na uamuzi huo mpya, ajira za walimu wapya wa masomo ya sayansi nazo zimebadilika kwani wale wote waliohitimu ualimu wa sayansi na hisabati, wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.
"Kuhusu wale walimu wa ‘arts’, kule tuna walimu wa ziada ambao tutajaribu kuwapanga kutokana na shule, kwani wengi walikuwa wamepangwa shule moja. Kwahiyo, tutaangalia utaratibu wa kuwapanga kulingana na mahitaji" .alisema Profesa Ndalichako.
Akizungumzia suala la ubora wa elimu nchini, Profesa Ndalichako aliwataka walimu wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu kwa kuwa wao ndio wanaowaandaa wanafunzi kabla hawajaenda vyuoni.
Chanzo:Mtanzania.
Akizungumza mjini Dodoma jana wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Profesa Ndalichako, alisema Serikali kwa sasa haiwezi kuajiri walimu wa masomo hayo kwa kuwa inataka kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ambao idadi yao ni ndogo.
Pamoja na uamuzi huo mpya, ajira za walimu wapya wa masomo ya sayansi nazo zimebadilika kwani wale wote waliohitimu ualimu wa sayansi na hisabati, wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.
"Kuhusu wale walimu wa ‘arts’, kule tuna walimu wa ziada ambao tutajaribu kuwapanga kutokana na shule, kwani wengi walikuwa wamepangwa shule moja. Kwahiyo, tutaangalia utaratibu wa kuwapanga kulingana na mahitaji" .alisema Profesa Ndalichako.
Akizungumzia suala la ubora wa elimu nchini, Profesa Ndalichako aliwataka walimu wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu kwa kuwa wao ndio wanaowaandaa wanafunzi kabla hawajaenda vyuoni.
Chanzo:Mtanzania.
Thursday, December 15, 2016
FREEMAXENCEMELO:"Sheria haishii kusema apelekwe Mahakamani ndani ya saa 24"-DPP afafanua sakata la Jamii Forum.
Wakati sakata la kukamatwa na kushikiliwa kwa Mkurugenzi wa kampuni ya inayomiliki mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo kwa siku ya tatu sasa likiendelea kutikisa vyombo vya habari ndani na nnje ya nchi,Mkurugenzi wa makosa ya jinai DPP Biswalo Mganga ametoa kauli ya serikali juu ya sakata hilo na kudai kuwa wanaweza kumshikilia kwa zaidi ya masaa 24 na kumuachia pale tu watakapoona wameridhika kuwa hana kosa lolote.
Chanzo:Azam Two.
Kanali wa Jeshi atoa ufafanuzi juu ya uteuzi wake NEC,siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM.
Wakati watu mbalimbali wakiwa na maoni tofauti kuhusu Chama cha
Mapinduzi (CCM) kupitia Halmashauri Kuu yake kumteua Kanali wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzaia (JWTZ) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa, mwenyewe ameibuka na kutolea ufafanuzi uteuzi
huo.
Kanali Ngemela Lubinga (katikati), kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omar.
Kanali Ngemela Eslom Lubinga amesema kuwa alishastaafu utumishi wake jeshini na kuwa angeweza kutumikia chama cha siasa kwani si mtumishi wa jeshi hilo tena. Kanali Lubinga aliyekuwa Msemaji wa JWTZ alisema kuwa alistaafu utumishi katika jeshi kuanzia Disemba 2 mwaka huu. Aidha, alisisitiza kuwa alijiunga na Chama cha Mapinduzi mwaka 1979.
Kikubwa kilichozua maswali kuhusu uteuzi huu ni kwa sababu wanajeshi na watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waraka wa Utumishi wa mwaka 2015 unakataza watumishi wa umma kuwa wanachama wa vyama vya siasa lakini unatambua haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Badhi ya maswali yaliyoulizwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni lini Kanali Lubinga alijiunga na CCM kiasi cha kuweza kuteuliwa katika nafasi ya juu kiasi hicho? Kama alijiunga na chama mwaka 1979 inaonyesha wazi kuwa alikiuka katiba ya nchi inayowataka wanajeshi kutojiunga na vyama vya siasa.
Akijibu swali hilo Kanali Lubinga alisema kuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja wanajeshi waliruhusiwa kujiunga na chama cha siasa na kuwa baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ndipo walizuiwa na kadi walizokuwa nazo zilichukuliwa.
Kanali Lubinga aliendelea kueleza kuwa kadi zile hazikutupwa bali zilihifadhiwa na hivyo baada ya kustaafu Disemba 2 mwaka huu akachukua kadi yake na kuendelea na uanachama wake.
Hata hivyo watu wa kada mbalimbali waliokosoa uteuzi huo wakitaka kuhakikisha kuwa siasa za nchi haziathiri utendaji wa majeshi yetu na utumishi wa watumishi wengine wa umma.
Kanali Ngemela Lubinga (katikati), kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omar.
Kanali Ngemela Eslom Lubinga amesema kuwa alishastaafu utumishi wake jeshini na kuwa angeweza kutumikia chama cha siasa kwani si mtumishi wa jeshi hilo tena. Kanali Lubinga aliyekuwa Msemaji wa JWTZ alisema kuwa alistaafu utumishi katika jeshi kuanzia Disemba 2 mwaka huu. Aidha, alisisitiza kuwa alijiunga na Chama cha Mapinduzi mwaka 1979.
Kikubwa kilichozua maswali kuhusu uteuzi huu ni kwa sababu wanajeshi na watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waraka wa Utumishi wa mwaka 2015 unakataza watumishi wa umma kuwa wanachama wa vyama vya siasa lakini unatambua haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Badhi ya maswali yaliyoulizwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni lini Kanali Lubinga alijiunga na CCM kiasi cha kuweza kuteuliwa katika nafasi ya juu kiasi hicho? Kama alijiunga na chama mwaka 1979 inaonyesha wazi kuwa alikiuka katiba ya nchi inayowataka wanajeshi kutojiunga na vyama vya siasa.
Akijibu swali hilo Kanali Lubinga alisema kuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja wanajeshi waliruhusiwa kujiunga na chama cha siasa na kuwa baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ndipo walizuiwa na kadi walizokuwa nazo zilichukuliwa.
Kanali Lubinga aliendelea kueleza kuwa kadi zile hazikutupwa bali zilihifadhiwa na hivyo baada ya kustaafu Disemba 2 mwaka huu akachukua kadi yake na kuendelea na uanachama wake.
Hata hivyo watu wa kada mbalimbali waliokosoa uteuzi huo wakitaka kuhakikisha kuwa siasa za nchi haziathiri utendaji wa majeshi yetu na utumishi wa watumishi wengine wa umma.
Wednesday, December 14, 2016
PICHA:Yaliyojiri kwenye ukaguzi wa Polisi kwenye ofisi za Jamii Forum na nyumbani kwa Mkurugenzi wa mtandao huo.
Mnamo tarehe 14 Disemba mchana Polisi kutoka kituo cha Kati, Dar es salaam
wakiambatana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Jamii Media,inayomiliki mtandao wa 'Jamii Forum' Ndugu Maxence Melo,
walifika katika ofisi za Jamii Media kwa ajili ya ukaguzi.
Zoezi hilo lilienda sambamba na kuwahoji wafanyakazi (Social Media Engagers na Content Quality Controllers) juu ya utendaji wa shughuli zao za kila siku ndani ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam na kuondoka na wafanyakazi wawili kwa mahojiano zaidi ambapo walielekea nyumbani kwa Maxence Melo kwa ajili ya ukaguzi ndani ya nyumba.
Katika zoezi zima la ukaguzi, sehemu zote mbili, Jeshi la Polisi halikuhitaji wala kuchukua kifaa cha mawasiliano ya kimtandao kama router, flash, hard disc, au kompyuta ila walichukua baadhi ya nyaraka za usajili wa kampuni hiyo.
Eneo la nnje la nyumba ya Maxence Melo.
Hata hivyo baada ya ukaguzi huo kwenye nyumba ya Bwn.Melo,msafara huo ulielekea kituo cha kati kukamilisha mahojiano kati ya Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wawili waliochukuliwa.
Credit:Mashuhuda wa SHILAWADU.
Zoezi hilo lilienda sambamba na kuwahoji wafanyakazi (Social Media Engagers na Content Quality Controllers) juu ya utendaji wa shughuli zao za kila siku ndani ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam na kuondoka na wafanyakazi wawili kwa mahojiano zaidi ambapo walielekea nyumbani kwa Maxence Melo kwa ajili ya ukaguzi ndani ya nyumba.
Katika zoezi zima la ukaguzi, sehemu zote mbili, Jeshi la Polisi halikuhitaji wala kuchukua kifaa cha mawasiliano ya kimtandao kama router, flash, hard disc, au kompyuta ila walichukua baadhi ya nyaraka za usajili wa kampuni hiyo.
Eneo la nnje la nyumba ya Maxence Melo.
Hata hivyo baada ya ukaguzi huo kwenye nyumba ya Bwn.Melo,msafara huo ulielekea kituo cha kati kukamilisha mahojiano kati ya Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wawili waliochukuliwa.
Credit:Mashuhuda wa SHILAWADU.
Mfahamu Edward Snowden,Jasusi wa CIA anaemuumbua Obama na ushahidi kuwa Osama Bin Laden yupo hai.
EDWARD SNOWDEN alizaliwa mjini North Carolina June 21,1983, babu yake (upande wa mama alikuwa admeri (Afisa darala la kwanza katika jeshi la majini) ambae baadae akawa afisa wa juu wa Shirika la kijasusi la Uingereza (FBI), bahati mbaya alikua mmoja wa wahanga wa mlipuko wa Pentagon 9/11. Baba'ke alikuwa mlinzi wa fukwe/pwani (Coast guard), mama'ke alikuwa msaidizi mkuu (chief assistance) mahakama ya jimbo la Maryland. Dada'ke alikuwa mwanasheria wa serikali. Akiwa katika umri mdogo kabisa (13), Snowden alipata alama zaidi ya 150 katika mitihani miwili ya kipimo cha IQ. Akiwa mdogo alipata ugonjwa aliomsababisha asiende shule takriban miezi 10, aliporudi shule alikuta mitihani ya GED akaifanya na kufaulu kwa wastani wa juu sana. Japo hakupata Bachelor degree, alifanikiwa kupiga Master's ya chuo kikuu cha Liverpool, Uingereza mwaka 2011. Akiwa na miaka 20 alitaja Ubudha (Buddhism) kama dini yake katika fomu za kujiunga na jeshi.
MTAZAMAO WA KISIASA WA SNOWDEN:
Snowden anadai kua uchaguzi wa 2008 (uliomweka Obama madarakani) alimpigia kura mgombea wa chama cha tatu (3rd-party candidate). Hakuamini katika falsafa za Obama na anadai kwamba alipanga avujishe siri za kijasusi za Nationa Security Agency (NSA) tangu 2009, lakini aliona busara avute subira akiamini kua Obama angetekeleza ahadi zake tofauti na Bw. G. W. Bush.
Baada ya kuvujisha siri nzito za kijasusi na usalama wa Marekani mwaka 2013, jukwaa la kijamii la Ars Technica lilithibitisha kuwa Snowden alikua active member wa jukwaa hilo na kwamba mwaka 2009 katika uzi unaohusu kulinda usalama wa taifa, Snowden alipost kwamba "I think leakers of classified information should be shot in the balls"-- "Nafikiri kwamba wavujishao siri nzito za taifa wapigwe risasi za korodani".
AJIRA:
May 2004, Snowden akiwa na miaka 21 aliorodheshwa kwenye kikosi cha akiba (US Army reserve). Alitamani sana kupigana vita ya Iraqi akiamini kwamba kupigana vita hivyo ni ishara ya ukombozi kwa watu wanyanyaswao, bahati mbaya hakufanikiwa kwakua alivunjika miguu akiwa kwenye mafunzo ya kijeshi.
2005 aliajiriwa kama mtaalamu ya maswala ya usalama katika chuo cha Maryland. Mwaka 2006 aliombwa ajiunge na CIA, ambapo aliwekwa kitengo cha mawasiliano ya kimataifa na upelelezi wa mtandao (network surveillance) makao makuu ya CIA Virginia. Mwaka huo alipost kwenye jukwaa la Ars Technica kuwa "siwezi kuhangaika kutafuta/kupata ajira kwakuwa mimi ni mchawi wa kompyuta", akiwa kijana mwenye umri mdogo zaidi katika timu ya wataalamu wa usalama wa mtandao, alipelekwa masomoni katika shule ya siri ya CIA kwajili ya kupata utaalamu wa hali ya juu ya kompyuta, ambapo aliishi hoteli yenye hadhi ya nyota 5 mwaka mzima akipata mafunzo hayo maalumu.
Mwaka 2007, CIA walimwagiza Snowden aende Geneva, Uswisi pamoja na jopo la wanadiplomasia kwajili ya kuchunguza na kuoperate usalama wa mtandao wa vikao vya siri. Alipewa pasi ya kusafiri ya Marekani daraja la diplomasia na alikabidhiwa apartment ya vyumba vinne karibu na ziwa Geneva. Akiwa kwenye hiyo trip, Snowden alishuhudia kwa macho jinsi CIA walivyoweza kuwahonga kwa rushwa kubwa mno maafisa wa benki ya dunia, maafisa wa ulinzi na wanasheria ili CIA waweze kujua siri za ndani za World Bank. Snowden alipigwa butwaa, kivipi Marekani ilikuwa inahubiri uwazi na kupinga vikali rushwa lakini kumbe ndani ya tundu la sungura wao wanatenda kinyume. Snowden alikasirishwa mno na tukio hilo.
Mwaka 2008 Snowden alichaguliwa na CIA aongozane na raisi Obama katika mkutano wa NATO huko Romania.ambapo mnamo Feb 2009, Snowden alimua kujiuzulu kua agenti wa CIA tayari akiwa na siri nyingi sana za ndani.
March 2009, alianza kazi kwenye kampuni binafsi la Dell ambapo alikua na wajibu wa kutoa maelekezo juu ya kuhakikisha usalama wa mitandao ya wateja wa Dell kuepuka cyber attack. Wateja wa Dell wakubwa walikuwa Yokota Air Base, Shirika la kijasusi la China, mashirika ya serikali na wizara mbali mbali za Marekani, CIA pamoja na kusimamia mifumo ya mawasiliano ya National Security Agency.
Upelelezi wa kitaalamu unaonesha kwamba Akiwa Dell, kuanzi April 2012, kwa kutumia ujuzi wake wa hali ya juu ya kompyuta, Snowden alianza rasmi kupakua mafaili ya siri za kiusalama za marekani ambazo inakadiriwa kufika zaidi ya documents million 1.
Akiwa analipwa mshahara wa mil. 420 tsh kwa mwezi, Snowden aliamua kuacha kazi katika kampuni ya Dell. Alikua na msukumo wa kumwaga siri zilizomchukiza za usalama wa dunia, lakini alisubiri apate pa kuanzia "breaking point". Siku ambayo kiongozi mkuu wa NSA Alipolidanganya Bunge la marekani (congress) na kula kiapo feki ndipo ilikuwa breaking point yake.
Mwezi mmoja baadae alitoroka marekani kuelekea Urusi ambapo alipewa hifadhi ya maficho (asylum) na Raisi Vladimir Putin. Baada ya kujihakikishia kuwa ana ulinzi imara ndipo Snowden alipoanza kurusha makombora kupitia mtandao wake maarufu wa Weakleaks.com,mtandao ambao umefungiwa nchini Marekani huku ukiwa na sifa ya kuandika habari nyeti zinzowahusu viogozi na watu mashuhuri Ulimwenguni.Kupitia mtandao huo alivujisha siri nzito sana za uwezo wa kivita wa marekani, silaha za kivita, tecknolojia, mbinu za kijeshi za marekani, oparesheni chafu za marekani. Katika historia ya ulinzi na usalama wa Marekani hajatokea mpuliza filimbi (whistle blower) aliyeweza kutoa siri nzito, za ndani zaidi na nyingi. Mwaka huo pekee Snowden alimpa mwandishi wa The Gurdian mafaili 10,000 ya siri. Pia njia nyingine aliyoitumia ni kufanya mahojiano na mwanahabaru sehemu ya siri na kisha kurushwa kwenye vyombo vya habari.
Snowden amekua akikutana na maafisa wa juu wa usalama wa nchi mbali mbali duniani kama Urusi, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Israeli na mshirika makubwa kama UN, World Bank, IMF na kuwaleza mipango ya Marekani kwa mataifa / mashirika hayo.
Kwasasa Snowden ni mmoja ya watu wanaoohitajika zaidi na Marekani, lakini ni ngumu kumdaka maana hata Mkurugenzi wa FBI James Comey aliwahi kusema... "Snowden akiwa CIA na NSA aliishi na magenius lakini wote kwake walikuwa ni taka taka". Unaambiwa Jamaa ana verified twitter account na huwa anarusha makombora mara chache chache.
LENGO/DHUMUNI KUU LA UZI HUU:
Mnamo mwaka 2011 serikali ya Marekani kupitia raisi wake Barack Obama ilithibitisha kwamba May 2 ya mwaka huo kikosi maalumu cha maangamizo kilifanikiwa kumtoa kwenye uso wa dunia adui namba 1 wa Marekani, Osama Bin Laden. Aliuwawa akiwa kwenye makazi yake Abboltabad, Pakistan kupitia oparesheni mkuki wa Neptune (Neptune spear) na mwili wake kuzamishwa baharini.
Daily mail waliandika kwenye kichwa cha habari "Kaoze kuzimu- Obama: Timu ya Wamarekani imemuua Osama kwenye pambano la moto"
May 2014, Snowden mpuliza filimbi, msaliti shujaa anaibuka kwenye mahojiano ya siri na kituo cha Moscow Tribune na kusema "The famous terrorist and former leader of Al-Qaeda is ALIVE and receives benefits from central intelligence Agency, CIA"-- "Gaidi maarufu na kiongozi wa Al-Qaeda yu hai na anapokea fadhila kutoka Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA).
Alienda mbali na kudai kuwa taarifa za kifo cha Osama zilighushiwa ili kumuongezea sifa na mvuto wa kisiasa raisi Obama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2012. Snowden anaendelea "I have classified documents showing that Osama is still on CIA's payroll"-- "Nina document murua zinazoonesha kwamba Osama bado yupo kwenye malipo ya CIA".
"He still receives more than $100,000 a week which are being transferred through some front businesses and organisations directly to his Nassau bank account, I am not certain where he is now, but in 2013 he was living quietly in Bahamas in his Villa with his 5 wives and many children"-- "bado anapokea zaidi ya mil 209 tsh kwa week kutoka CIA, ambayo inahamishwa kibiashara na mashirika moja kwa moja kwenye akaunti yake ya benki ya Nassau. Sina uhakika alipo sasa, lakini mwaka 2013 alikuwa anaishi maisha ya kifahari sana Bahamas yeye na wake zake wa5 pamoja na watoto wake wengi"
Snowden alidai kwamba "Osama bin Laden" ni mshirika (operative) mtiifu na makini wa CIA kwa muda mrefu sasa. Je tukio la Marekani kumuua Osama lingefikisha ujumbe gani kwa washirika pandikizi wa CIA? Kwamba nao wajiandae kuuwawa? Anaendelea kudadavua kwamba Marekani ilipanga shambuluo la bandia la kumuua Osama kushirikiana na Pakistan Secret service na hili tukio limemkumbatia Osama na kumfanya awe salama zaidi, kwasababu kila mtu ameamini Osama ameuwawa, hivyo hakuna mtu atakayejishughulisha kumsaka.
Leo hii Snowden akiwa na makosa yenye kifungo cha jumla ya miaka 120 yupo mafichoni katika nchi za Urusi na Brazil. Baadi ya watu wanamuona kama Msaliti wa usalama wa taifa na baadhi ya watu wanamuona ni mwananchi mzalendo.
UKWELI UNAOTHIBITISHA KUWA OSAMA HAKUUWAWA KWENYE OPARESHENI GERAMINO.
☆Kivipi Osama afe mara mbili, ni lini alifufuka?
Wachambuzi wa maswala ya kijasusi, viongozi wa nchi, wakuu wa taasisi za usalama waliwahi kuzungumza kwamba Osama alifariki miaka mingi iliyopita (2001). Afisa veterani wa CIA Robert Beir, kiongozi wa zamani wa FBI kitengo cha kupambana na ugaidi (counter - terrorism, waziri mkuu wa zamani wa Pakistani Banazir Butto, Alex Jones wa CIA wote walidai Osama alifariki 2001. Katibu mkuu msaidizi wa Marekani Dr. Steve Pieczenik aliwahi kuthibitisha kwamba Osama alifariki kwa ugojwa wa 'Marfan Syndrome' na kwamba daktari wa CIA walifika kuupima mwili wa Osama akiwa hospitalini Dubai.
☆Mkanganyiko wa matukio ya oparesheni Geramino.
Kwanza tunaambiwa kulikuwa na majibizano ya risasi ya dakika 40, tena tunaambiwa hakukuwa na majibizano yoyote (kwamba mlinzi m1 wa Osama alitandikwa mkwaju akafariki na kisha kikosi cha FBI kikamfikia Osama.)
Tunaambiwa Osama alijeruhiwa vibaya, mara tena tunaambiwa Osama hakujeruhiwa bali alimtumia mkewe kama ngao.
Tunaambiwa makazi ya Osama yalikuwa ya ghali zaidi ya $1 million, ukweli ni kwamba kilikuwa ni kakibanda cha ovyo hata hakifiki robo ya hiyo pesa.
Taarifa alizotoa Obama na maafisa wa usalama na intelijensia zilikuwa zinapishana sana.
☆Kutupa mwili wa Osama baharini.
Baada ya watu kushambulia kitendo hicho, Obama aliibuka na kusema kwamba walifanya hivyo kufuata utaratibu wa Ibada ya mazishi ya kiislam. Lkn wanazuoni wa kiislam wakapinga vikali hoja hiyo wakidai kwamba muislam anaweza tu kuzikwa baharini endapo alifia baharini.
☆Uchunguzi wa sayansi wa vinasaba na sura.
Viongozi wa usalama walidai kwamba vipimo ya DNA na uchunguzi wa sura (facial recognition) vilifanyika ili kuhakiki pasi shaka kuwa mwili ule ulikua ni wa Bin Laden. Je ni kwanini vithibitisho hivi havijawahi kuwekwa popote hadharani?
☆Kughushi picha ya chumba cha matukio (situation room).
Ikulu ilitoa picha ikimuonesha rais Obama,Waziri wa mambo ya nnje H. Clinton, Makamu w rais Joe Biden na staff wengine wa ulinzi wakifuatilia shambulio lililomuuwa osama. Lakini baadae mkuu wa CIA, Leone Panette alikiri wazi kuwa Obama na team yake wasingeweza kushuhudia shambulio hilo 1 kwa 1 (live feed) kwani mitambo ya kurekodi tukio hilo ilizimwa ili isiingiliane na mawasiliano eneo la tukio.
Picha hii iliundwa mahsusi kumpa obama kiki ya kihistoria.
☆Tamko la Al-Qaeda.
Vyombo vya habari viliripoti kua Al-Qaeda wenyewe wamethibitisha kuuwawa kwa Osama. Lakini mchezo huu ulisukwa na shirika liitwalo SITE ambao ni mtandao maalumu wa kupika propaganda za shambulio la Pentagon. SITE ipo chini ya binti wa shushushu wa Israel mara kadhaa wamekuwa wakidakwa kutengeneza video kwa kutumia utaalamu wa juu kulingana na matakwa ya serikali.
☆Majirani wa mjengo wa Osama.
Majirani wa Osama ktk kijiji cha Abboltabad hawajawahi kuhisi tetesi zozote juu ya uwepo wa Osama hapo. Hata jeshi ya Pakistani ambalo lipo jirani walishindwa kung'amua uwepo wa Osama pia. Obama pia alithibitisha kua hawakuwa na uhakika 100% kuwa Osama alikuwa ndani ya lile jengo (ni kama kamari). Yawezekana aliuwa mtu tofauti kabisa na kuamua kuutangazia ulimwengua kuwa wamemuuwa osama ili kuficha aibu.
☆Osama alikuwa ni asset.
Asset katika dunia ya kiinteligensia ni kitu chochote chenye thamani/value ya kuweza kudukua taarifa muhimu. Inadaiwa gaidi aliyekamatwa porini ndiye aling'amua wapi Osama alipo baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa mateso (torturing interrogation) ndipo akafunguka. Iweje Osama ambaye alikuwa gaidi most wanted na biggest asset asikamatwe ahojiwe ili kung'amua taarifa za ugaidi wa ulimwenguni. Moja kwa moja aliuwawa wakati lengo la Marekani lilikuwa kumkamata akiwa hai (kwanini walimuuwa wakati kulikuwa na uwezekana wa kumkamata akiwa hai).
Swali la kujiuliza je ni kweli Osama alikua na ulinzi dhaifu kiasi kile? Ni kwanini marekani walifanya shambulio hili bila kuwashirikisha viongozi wa usalama wa Pakistan.
HITIMISHO:
Obama, ikulu ya marekani, taasisi na mashirika ya ujasusi ya Marekani na viongozi wa usalama wa Marekani hawajawahi kutoa tamko la kupinga/kukanusha filimbi aliyopuliza Bw. Snowden (Obama alijitahidi kujibu baadhi ya hoja za Snowden lakini kamwe suala la kifo cha Osama hajawahi kulizungumzia au kukanusha).
Credit:Wikipedia-Daily Mail-Weakleaks-CNN-Mabalozi wa SHILAWADU.
WAFUASI WA CUF WATWANGANA MAKONDE MAHAKAMNI TENA.
Wafuasi wa CUF watwangana tena mahakamani
Monday, December 12, 2016
Kutana na Jambazi mtoto aliefunga mtaa jijini Mwanza na kupora fedha.
Mtoto anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 15-17 amefunga Mtaa wa Mecco, Kata ya Nyakato wilayani Nyamagana, Mwanza kwa kupiga risasi hewani na kusababisha taharuki kubwa kwa wafanyabiashara na Wananchi.
Tukio la kijana huyo ‘kufunga mtaa’ limetokea usiku wa tarehe 11Disemba 2016 saa 1:45 katika Mtaa wa Mecco stendi, baada ya (kijana) huyo kutaka kupora katika duka moja linalouza mtungi ya gesi na vifaa vingine.Hata hivyo, katika mapambano ya wawili hao, kijana huyo alianza kupiga kelele zilizosikika, ‘niachieni, niachie’ huku mfannyakazi wa duka hilo akiomba omba msaada kwa watu waliokuwa karibu na duka hilo.
Baada ya watu kufika huku mfanyakazi wa duka hilo, akiita ‘mwizi mwizi,’ watu walifika na kumshika kijana huyo ambapo hata hivyo kijana huyo aliwaponyoka na kutoa silaha iliyokuwa kwenye begi na kupiga risasi moja hewani kuwatawanya watu waliokuwa eneo hilo kutawanyika.
Baada ya kijana huyo kupiga risasi hiyo hewani,gari ndogo nyeupe aina ya 'Saloon' ilifika na kumchukua na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wananchi wa eneo hilo kupigwa butwaa.
Daud Machota, mmoja wa Wananchi wa eneo hilo amesema kuwa, vitendo vya uhalifu katika eneo hilo vimeanza kutishia amani kwani kumesababisha watu wengi kulala mapema.
“Kwanza mimi ninachoshangaa inakuaje mtoto mdogo wa miaka 15 – 17 anashika silaha na kupiga risasi hewani, labda hawa watoto wanaweza wakawa wamefunzwa mafunzo ya kigaidi, haiwezekani kwa umri wake kufanya hivyo,” amesema Machota.
Machota amesema kuwa, kijana huyo alifanikiwa kuchukua kiasi cha Sh. 40, 000 kwenye duka hilo, huku akidai kwamba uhalifu huo unasababishwa na ugumu wa maisha unaonekana kuwagusa watu wengi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza na Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai kuwa, askari walikuta katika eneo la tukio begi na shati moja.
“Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika uhalifu huo, tunaendelea na uchunguzi kuwakamata watu wanaofanya vitendo hivyo, ilipigwa risasi moja hewani,” amesema Msangi.
Chanzo:Mashuhuda wa SHILAWADU,Mwanza.
Sunday, December 11, 2016
PICHA:SHEKH PONDA AMTEMBELEA MBUNGE GODBLESS LEMA GEREZANI NA KUMUUSIA MAMBO MAZITO.
Mwenyekiti wa zilizokua Jumuiya za kiislamu nchini Shekh Ponda amtembelea mbunge wa Arusha Mjini Godbless J Lema, ktk gereza kuu la Arusha Kisongo leo, na kusema Haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote.
Pia alimtia moyo Lema na kumwambia sikupi pole nakupa hongera haya unayoyapitia niliwahi kupitia lkn usirudi nyuma songa mbele
Shekh Ponda akiwa na ndugu kutoka familia ya Mh.Lema
Lema ambae ni mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),amekua akishikiliwa na vyombo vya usalama akituhumiwa kutamka maneno ya uchochezi baada ya kudai kuwa ameota ndoto kuwa endapo Rais Magufuli asipojirekebisha atakufa
.
Tuesday, December 6, 2016
ZITTO KABWE AHUSISHWA SAKATA LA MANJI KUTIMULIWA QUALITY PLAZA.
Uamuzi wa kuyatimua makampuni ya mfanyabiashara Yusuf Manji, Diwani wa Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, unafuatia uamuzi wa shauri lililokuwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ambao ulitolewa na Jaji Mgetta Novemba 24, 2016, ambapo pamoja na mambo mengine, iliamuliwa kampuni hizo ziondoke mara moja kwenye jengo la QUALITY PLAZA.
Notisi hiyo ya masaa 24 ilizitaka kampuni zilizoko kwenye jengo hilo katika Kitalu Namba. 189/2 kwenye Barabara ya Nyerere kuwa ni Quality Group Company Limited, Gaming Management Limited, Q Consult Limited, Quality Logistics Company Limited na International Transit Investment Limited, ambazo ziko chini ya Manji kuondoka mara moja.

Hata hivyo sakata la Manji kutimuliwa lilianza kitambo akidaiwa kufanya biashara zenye utata na mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kufanikiwa kuiuzia PSPF jengo la Quality Plaza na Mufuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) maghala kwa shilingi bilioni 46, ambayo aliyajenga kwa mkopo wa Sh bilioni 9 kutoka mfuko huo.
Kumbukumbu za SHILAWADU zinaonesha kuwa ijumaa ya Mwezi wa 4 ,2011 PSPF ilifanya maamuzi kama hayo baada ya kubanwa na Wabunge wa Kamati Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) enzi hizo sasa (PAC),iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ,ambae kwa sasa ni Mbunge wa Kigoma mjini (ACT).
Thursday, November 17, 2016
ANGUKO LA MABENKI:Barclays yatoa tahadhari kwa watumishi wake.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya mabenki ukiacha enzi zile za Meridian Biao, ni wazi sekta ya benki nchini inapitia hali tete hii ikiwa ni baada ya benki kongwe ya Barclays tawi la Tanzania kutoa taadhari kwa wafanyakazi wao kwamba benki yao inapitia kipindi kigumu kifedha hivyo kuamua kufuta baadhi ya shughuli ndogo kabisa kama sherehe za 'Family Day'.
Taarifa imekuja baada ya benki ya CRDB nayo kutoa mchanganuo uliobaini hasara ya bilioni kwenye .hesabu zake za robo mwaka (Quarterly Financial Statements).
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
facebook

















