Thursday, August 30, 2012

UNAIJUA HII!! AKIWA NA MIAKA 82 HATIMAYE HATUNAYE TENA!

NEIL AMSTRONG MWANADAMU WA KWANZA KUKANYAGA MWEZI.

Neil Amstrong amefariki dunia baada ya kutokea complications akifanyiwa oparation ya moyo .Neil Amstrong amefariki akiwa na miaka 82.Dunia itamkumbika kwa rekodi yake ya kihistoria ya kuwa binadamu wa kwanza kuingia na kukanyaga mwezini.
Mission hiyo ya Apollo 11 ilifanyika mwaka 1969 na yeye akiwa kiongozi wa msafara wa watu watatu kuelekea mwezini.
 Ilikuwa  july 6 1969 wakijiandaa kuondoka huku wakipunga kuaga na yeye mbele kabisa kuingia kwenye van iliyowapeleka kwenye rocket tayari kuanza safari kuelekea mwezini.
 Neil Amstrong kushoto na mwenzake Buzz Aldrin kushoto wakiwa tayari mwezini na kuweka bendera ya Marekani.Walikaa mwezini kwa masaa matatu tu.
 Neil Amstrong alikanyaga kwa mara ya kwanza mwezini yeye akiwa wa kwanza July 20 1969
Alama hiyo ya mguu inaonyesha jinsi gani mwezini ni kama ardhi  laini sana kama poda hivi.
 Buzz Aldrin yeye alikuwa wa pili kukanyaga mwezini nyuma ya Neil japo wote walikuwa katika mission moja hiyo ya Apollo 11.
Marehemu Amsrong akiwa na Presidaa Barack Obama 09.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.