Saturday, November 3, 2012

Baguje "Huyu Ndie Mrithi wa Matonya, Suma Lee, Bwana Misosi na wengine wote waliowahi Kuiteka Tanga na Style zao za Uimbaji"

Bagujeee
Utakaposkia Ngoma yake ya kwanza "Ng'aNg'a" hautopingana na Kauli yangu kuwa ni Moja kati ya wauza sauti ng'ang'aa kwa mwaka 2012, amezaliwa na kukulia katikati ya Jiji la Tanga, na Tamasha la Fiesta Linaloandaliwa na Cloudsfm Radio kupitia kwa watangazaji wa Kituo hicho Diva Loveness Love na Adam Mchomvu na kwenye Mabano Fundi Mitambo Gossip Cop Soudy Brown, wakiwa Mkoani Tanga kwa Pamoja baada ya kumskia Baguje anaimba Acapella katikati ya Kundi la watu wakakiri kuwa Kijana iwapo ata record ngoma na ikijumuishwa kwenye PlayList za radio basi ngoma hiyo itakidhi kiu ya kiburudani ya Mtanzania, kumbe tyme hiyo Baguje alikua ana Ngoma yake Kibindoni,
Kwa mara ya Kwanza baguje ali perform kwenye Jukwaa la Fiesta Tanga 2012, baadae akaja kushare na Stage moja na Mic Moja na Msanii wa kimataifa Ricky Rozay kwenye Serengeti Fiesta 2012 Dar es salaam
Huo ndio mwanzo wake anasema tutegemee mengi kutoka kwake
Enjoy Ngoma yake ya kwanza hii hapa:

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.