B-Boy-Stereo |
Baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu na Record Label
ya M Lab chini ya Patrick Gondwe na Producer Duke Tachez, na ndani ya mkataba huo akafanikiwa kurelease
album moja ya African Son pamoja na kushiriki kwenye Mixtapes kadhaa, Stereo
alifunguka kuwa yuko huru na iwapo kuna management itavutiwa kufanya naye kazi
ye yuko poa, baadae kukawa na rumorz kuwa bonge la bwana Sheta anamnyemelea Stereo
ili ikiwezekana amsign, na ki ukweli mara kwa mara walikua wana hang pamoja
Ila hivi karibuni tukaskia Stereo yuko chini (Unity Entertainment)
ya mshindi wa tuzo ya Channel O Music video awards, Ambwene Yesaya A.Y , na mkataba huo ulisainiwa Tarehe 12 mwezi wa 12 mwaka 2012 jioni, mbele ya macho ya Mwanasheria Anna Mwakatundu, Arthur Samuel A.Y na Stereo mwenyewe
Mskize Stereo alivyo Tiririka ndani ya 255 ya XXL/ Cloudsfm: