Wednesday, November 16, 2016

INSTAGRAM:Lady Jay Dee afunga ndoa tena.




Msanii nguli wa muziki kwa upande wa Wanawake nchini,Binti Komando,Lady Jay Dee amefunga ndoa kwa mara pili na hii ikiwa ni baada ya kupost ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika "Big shout out kwa Coastal air kwa kufanikisha safari yangu kwenda honeymoon #ZanzibarIsland".

Mashabiki wa Mwanamuziki huyo wameoneshwa kufurahishwa na hatua hiyo,huku wengine wakitaka kumfahamu mwanaume huyo mpya alienasa kwenye moyo wa Jide anaetamba na wimbo wake mpya 'Sawa na wao'.


Awali mwanamuziki huyo aliolewa na Mtangazaji maarufu wa redio nchini Gadner G.Habash,kabla ya mgogoro wa muda mrefu uliopelekea kila mmoja kuchukua hamsini zake.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.