Wednesday, November 16, 2016
PICHA:Barabara ya bilioni 4 za sherehe za Uhuru kama inavyoonekana kutoka angani.
Wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru Disemba 9 mwaka huu,Rais Magufuli alifuta sherehe za uhuru na kuagiza kiasi cha fedha takriban bilioni 4 zilizopangwa kuratibu sherehe hizo kutumika kwenye mradi wa upanuzi wa barabara eneo la kutoka Morocco hadi Mwenge jijini Dar es salaam,huku akiwataka wananchi kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa taifa letu kwa kufanya usafi kwenye maeneo yao.
Huu ni muonekano wa juu wa barabara hiyo iliyopanuliwa na kuruhusu magari mawili kwenda na kurudi kwa wakati mmoja.
Comments System
facebook
