Wednesday, November 16, 2016

Kizungumkuti cha fedha za misaada kwa waathirika wa tetemeko kutafunwa;Serikali yatoa ufafanuzi.


Baada ya mijadala mingi kuhusu michango kwa waathirika wa tetemeko mkoani Kagera, serikali imetoa ufafanuzi kuhusu michango hiyo.

Serikali imesema imeshapokea misaada ya Vifaa, Chakula, Fedha na ahadi zenye thamani ya Sh. bilioni 15.19 kwa ajili ya Wahanga wa Tetemeko mkoani Kagera.

Zinahitajika jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 104.9 kwa ajili ya kukabiliana na maafa ya tetemeko ili kuurudisha mkoa huo katika hali yake halisi.

Pia imesema kuwa baadhi ya nchi zilizotoa ahadi kama Serikali ya Uingereza, wameahidi kutekeleza ahadi hiyo kwa kujikita moja kwa moja katika ujenzi wa shule zilizoathiriwa na tetemeko hilo.






Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.