Wednesday, November 9, 2016

Lukaku kuhama Everton..!

Mshambuliajj huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Klabu hiyo kwa mkopo mwaka 2013 kabla ya kujiunga rasmi na klabu hiyo kwa kitita kilichovunja rekodi cha pauni milioni 28 mwezi Julai 2014.



Licha ya kuwasilisha ombi la kuhama msimu uliopita ,Romelu Lukaku amefunga mabao saba kati ya 15 yaliofungwa na Everton katika ligi msimu huu.




''Iwapo Romelu angeendelea kucheza Everton hadi mwisho wa wakati wake najua angeacha kitu nyuma''......''Uwezo wake ni mkubwa na juu zaidi ya Everton'' anasema Kocha wake,Ronald Koeman.


Hata hivyo Everton imesema kuwa iko tayari kumpatia Lukaku kandarasi ya muda mrefu na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo.

-BBC.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.