Wednesday, November 16, 2016

Rais Kabila atangaza kutowania urais kwenye uchaguzi ujao 2018.

Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Joseph Kabila, amewahakikishia raia wake kwamba ataheshimu Katiba ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao unaotegemewa kufanyika mwaka 2018.


Akilihutubia Bunge la nchi hiyo, Rais Kabila ameomba kuwepo amani na utulivu.

"Kwa wale ambao wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, ninasema asante lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongomani" Alisema Kabila.

Jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.

Hatua hii ni ya kutuliza msukosuko wa kisiasa nchini DRC baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.


Chanzo:BBC.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.