Thursday, April 5, 2012


Rais mpya ambaye alichaguliwa hivi karibuni nchini SENEGAL ,MACKY SALLY hatimaye amemteua mwanamuziki maarufu nchini humo na dunia nzima kwa ujumla YOUSSOU NDOUR kuwa waziri wa utalii na utamaduni


YOUSSOU NDOUR alikuwa na nia ya kugombea nafasi ya urais nchini humo lakini baadae akajitoa katika kinyang’anyiro hicho ambacho kilimuinua MACK SALLY kuwa rais katika duru ya pili ya uchaguzi na kumshinda mpinzani wake aliyekuwa rais wa nchi hiyo ABDOULAYE WADE.

YOUSSOU NDOUR ni mmoja kati ya mawaziri 25 waliochaguliwa ambao wanaongozwa na waziri mkuu aitwae ABDUOUL MBAYE.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.