Saturday, February 16, 2013

YOUNG TUSO ADONDOSHA REMIX YA NDIO MZEE BY PROFESA JAY, ISKIZE KISHA #TIRIRIKA

Young Tuso
Yapata Miaka kumi na mbili imepita Tangu The Heavy Weight Mc Profesa Jay apate Tuzo ya Mtunzi Bora  wa Hip Hop nchini Tanzania kupitia Ngoma yake ya Ndio Mzee aliomshirikisha Juma Nature pamoja na Lady Jay Dee, chini ya Mtaarishaji Mahiri wa Bongo Flava P Funk Majani wa Bongo Records, Leo msanii mwingine Namzungumzia YOUNG TUSO anayewakilisha wilaya ya Temeke, ambaye enzi zile alikua Darasa la Tatu ameurudia wimbo huo na kutupia Ujumbe mpya ambapo vingi vilivyozungumzwa vinahusiana na mazingira ya sasa ya Sanaa kwa Ujumla nchini Tanzania, kwa mfano kuna Ma star ambao amewataja enz zile za Ndio Mzee Original (2001) walikua bado hawajawa Nyota.
Mwaka 2010 Tuso aliwahi kutoa Remix ya Bado Nipo Nipo By Mwana Fa
Tuso pia mwaka 2012 Amewahi kutoa Ngoma zake kama Jackline Wolper ambayo alizungumzia jinsi anavyompenda Star wa Bongo Movie Jackline Wolper, Ngoma nyingine inaitwa Yupi Bora Featuring ALi Kiba (2011)
Skiza Mahojiano aliyofanya Young Tuso Na Makorokocho Fm:




Skiza na Ndio Mzee Remix By Young Tuso:



Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.