Kutoka kulia ni Kajala na Aunty Ezekiel katika Party ya kumkaribisha KAJALA Uraiani iliyofanyika Ambassador Lounge |
Star wa Bongo movie aliyenusurika kifungo cha zaidi ya miaka mitano jela, baada ya kulipiwa fine ya milioni 13 na Star mwingine wa Bongo movie Wema Sepetu, hivi karibuni kupitia kipindi cha XXL ya Cloudsfm ametiririka Pyaaaaa... kwamba eti wakati akiwa Jela/ segerea, yeye na mfungwa mwenzake Lulu pamoja na wafungwa wenzao enzi hizo wakiwa Jela walikua wakihakikisha hawakosi kuskiza kipengele cha YOU HEARD / XXL ili kupunguza stress na kujua kinachoendelea mitaani, kwa bahati mbaya kuna majanga yakatoke maskina kina Kajala wakapokonywa radio yao na askari jela mnoko basi wenyewe walikua wanakonda sanaaaaa, binafsi kabla Kajala hajatoka jela niliwahi kupenyezewa taarifa hizo na Askari jela flani mshkaji wangu lakini kama nilikua siamini amini hivi, ha ha ha u spoon tenaaa, Asanteeee Karibu mtaani Kajalaaa VINGINE MWACHIE BABA NA MAMAAA
SKIZA KAJALA ANAVYOTIRIRIKA HAPO CHINI: