Tuesday, May 28, 2013

ALBERT MANGWEA A.K.A NGWEA AFARIKI DUNIA SOUTH AFRICA

1 Picha ya Ngwea akiwa South Africa kabla ya kifo chake
2 Picha ya Ngwea akiwa South Africa kabla ya kifo chake

Zaidi ya masaa matatu yaliyopita katika jamii ya watanzania wanaoishi South Africa zilisambaa taarifa kuwa msanii wa Muziki wa Kizazi kipya /  bongo flava anayefahamika kama Albert Mangwea a.k.a NGWEA amefariki dunia akiwa hospitali Hellen Joseph Hospital iliyoko jijini JO BERG , taarifa hizo zikasambaa hadi tanzania, ndipo tukajaribu kucheki na watanzania wanaoishi nchini humo na kuwapata baadhi ya washkaji ambao alikua akiishi nao pamoja, tulizungumza na mshkaji mmoja jina tunalihifadhi akasema kwamba Ngwea alirudi jana usiku akiwa mzima huku akiwa ameongozana na msanii mwingine wa bongo flava wa siku nyingi nae anafahamika kama M TO THE P wakalala, asubuhi kulipokucha jamaa akawa amelala fofofo, wakajaribu kumwamsha na kumwagia maji bila mafaniko ndo ikabidi wamwahishe hospitali madaktari wakajaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio, ndipo madaktari wakatoa ripoti kuwa msanii huyo ameaga dunia.
skiza mazungumzo kati ya muhariri wa gazeti la makorokocho na rafiki wa Ngwea anayefahamika kama GoodLuck.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.