Baada ya kuwepo rumors kuwa RnB Singer Ben Pol ame copy na kupaste wimbo wake mpya alioutoa hivi karibuni "Jikubali" fununu zikasambaa mtaani kuwa eti ngoma hiyo inafanana na wimbo unaoitwa Hall of Fame uliotoka mwezi wa nane mwaka 2012 na kuimbwa na kundi linaitwa The SCRIPT wakiwa wamemshirikisha
Will.i.am , sasa Ben PoL amepangua shuti na kusema kuwa haujui huo wimbo, na yeye hajacopy kokote, ila alichofanya wakati ana record ngoma hiyo mpango wake ulikua ni kufanya wimbo wenye melody nyepesi na anahisi ndio maana watu wanaufananisha na "Hall of Fame", Ben akaongeza kuwa wimbo wake haufananishwi tu na Hall of fame bali kuna nyingine kama tatu zaidi watu wanamwambia zinafanana na ngoma yake, na yeye kabla ya kuutoa alijua tu akifanya Melody nyepesi kama hiyo ambayo hata mtoto rahisi kushika basi yatasemwa mengi.
Na kwa mujibu wa changamsha genge za mtaani , zinadai kuwa eti kuanzia Idea ya kinachozungumziwa ndani ya nyimbo hizo mpaka melody zake zinafanana kinoma noma.
Iwapo itathibitika kuwa Ben PoL amecopy na kupaste ngoma yake, basi itakua ni aibu na kashfa kubwa kwake kwani kwa sasa hivi ndo anachukuliwa kama ndo msanii mkali wa RnB Tanzania yani kama taji la ufalme wa RnB bongo basi yeye ndo analishikilia na wengine wanafata kama Belle 9 na wengineo.
Ben PoL pia ametajwa mara 5 katika categories mbalimbali za Kili music awards.
Source: Gazeti la Makorokocho.
Iskize JIKUBALI YA BEN POL:
KISHA ULINGANISHE NA UNACHOKISKIA KATIKA VIDEO HII :