|
Mesen Selekta |
Jana kama uliskiza You heard ya XXL on clouds fm ulimskia dada mmoja jina tunalihifashi alidai kuwa mwezi mmoja uliopita Producer Mesen Selekta jina la passport Jerry Katoto ametoroka hotelini kwao na deni la zaidi ya laki tatu kwani aliishi hotelini kwa zaidi ya wiki tatu, mwanadada huyo alidai kuwa bosi wa hoteli hiyo amepanga kumkata mshahara yeye na mwenzake kwa kusababisha hasara hiyo, jana Mesen hakuweza kupatikana lakini leo mtaarishaji huyo wa muziki na mmiliki wa studio za Defetality zilizoko Sinza, ametiririka kuwa hausiki na deni hilo kwani yeye mwanza aliitwa na washkaji flani kwa ajili ya kwenda kuwafungia vifaa vya studio na washkaji hao ndio waliokwenda kufanya booking hotelini kwa hivyo ishu ya malipo inawahusu wenyeji wake, Mesen ameongeza kuwa hakutoroka hotelini bali alipatwa na dharura ikabidi arudi Dar es salaam ghafla.
Skiza You Heard ya XXL