|
Lamar katikati akiwa na wanadada wanaounda kundi la SHOSTEES/
hii ilikua ni front page ya magazine ya mzuka |
Baada ya kufanikiwa kuwatoa wanadada watatu wanaounda kundi la Shosteez Producer Lamar wa Fish Crab Audio Station ameona utamu na sasa hivi ameamua kutoa mchongo mwingine kwa vijana wengine wenye Vipaji na tyme hii mzazy anaangazia zaidi kwa vijana wa kiume hata wa kike wakijitokeza si mbaya ila anachotaka ni kuunda kundi BOY BAND, Lamar amesema kwa wavulana wanatakiwa wawe wanafanya typical RnB na wajue kucheza kama chriss brown na Neyo, na kwa wasichana wanatakiwa wawe kama rihanna, beyonce, kate perry, umri kuanzia miaka 18-25 , kama una vigezo hivyo mtumia kazi zako Lamar kwa Email : fishacrabmusic at gmail.com au fikisha demo yako studio Kariakoo.
Kundi la Shostees japokua lina muda mfupi tangu lianze lakini mafanikio yake ni makubwa kulinganisha na makundi mengine, wamefanikiwa kutokeza kwenye front page ya Mzuka Magazine, lakini pia inadaiwa kuwa wamepata deal kubwa kutoka kwenye kampuni kubwa ya vinywaji duniani yenye tawi lake tanzania pia nazungumzia Coca Cola, wanadada hao pia wametoa Audio moja na video, kama vp piga chabo hapo chini: