Ilunga Khalifa ‘Cpwaa’ |
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Ilunga Khalifa ‘Cpwaa’,
ameanzisha ‘lebo’ yake inayojulikana kwa jina la ‘Brain Storm Music’
ambayo tayari ameanza kusajili wasanii mbalimbali.
Kwa mujibu wa Cpwaa, kupitia ukurasa wake wa facebook, ameamua
kufanya hivyo kwa lengo la kuwapa sapoti wasanii wa bongo katika muziki
huo ili uweze kuwa wa kimataifa kama ilivyo katika nchi za wenzetu.
Alisema kuwa lebo hiyo itakuwa inafanya kazi ya kumtangaza msanii,
kurekodi video na ‘audio’ za wasanii ambao wapo kwenye mkataba na lebo
hiyo kama zilivyo za kimataifa kama ‘Young Money’, ‘Cash Money’, ‘MMG’,
‘Nad Boys’ na nyinginezo.
“Nimefungua lebo yangu hivi karibuni, sasa hivi nipo nasajiri wasanii
mbalimbali, hii itakuwa inajitegemea bila kushirikiana na kampuni
yoyote na itasimamia kazi za wasanii ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe,”
alisema.
Msanii huyo alisema kwa sasa bado hajataka kuwaweka wazi wasanii
ambao wameingia nao mkataba, kutokana na taratibu kutokamilika na
kwamba, baada ya kukamilisha wote watakuwa wazi.
Cpwaa ni kati ya wasanii wa Bongo ambao wanafanya muziki wao vizuri
na kujulikana kimataifa, kutokana na ubora wa uongozi ambao unamuongoza
katika tasnia hiyo.
Tanzania Daima