Makala hii aliiandika siku ya mwanamke dunia tarehe 8 mwezi wa 3
Tafiti zinaonesha kuwa kidunia kila mwaka wanawake 529,000 hufariki
dunia kutokana na matatizo ya uzazi wakati wa kujifunguwa ama wakati wa
ujauzito. Tanzania ni Moja Wapo kati ya nchi 10 zinazo changia asilimia
60 ya vifo hivyo,
Katika kila wanawake 100,000 watarajiwao kujifungua nchini Tanzania
wanake 454 hufariki dunia, sawa sawa na wastani wa wanawake 32 kila
siku.
Kwa maana kwamba imechukuwa miaka 10 (toka mwaka 2004 mpaka 2014)
kupunguza vifo vya wana wake kutoka vifo758 kati ya wanawake 100,000
wanao kuwa kaitika Hali ya kujifunguwa ama uja uzito, mpaka kufikia
vifo 454 Kati ya wanawake 100,000 wanao kuwa katika hali ya kujifunguwa
ama uja uzito. kwa kweli hii ni speed ya konokono Ama speed ya trector
kama nilivyo imba katika kibao changu cha bei ya mkaa. Ikiwa umebaki
mwaka mmoja tuliotakiwa kufikia malengo ya millenia ya kutokomeza kabisa
vifo vitokanavyo na uzazi na ujauzito
Haki namba moja ya binadamu ni haki ya kuishi, kwa mtizamo wangu mimi
vifo hivi vya kina mama ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, kwa
sababu vifo hivi vinazuilika na sio bahati mbaya kama wengi wetu tunavyo
dhani ama tunapokuwa tuna ripot habari ya mwanamke kupoteza maisha
kutokana na matatizo ya ujauzito ama uzazi
“Mwanamke anapofariki kutokana na matatizo ya uzazi ama uja uzito
siyo bahati mbaya bali ni uhalifu utokanano na ukosefu wa haki za
kijamii ( social in justice )” mfano 50% ya wanawake hujifungulia
nyumbani hali ambayo hupelekea vifo vingi haswa vijijini ambao wengi wao
ni wasichana wadogo wa uzazi wa kwanza ambao mara nyingi huwa na
changamoto nyingi zinazo hitaji uangalizi wa kitaalamu. 75% ya vifo
hivyo vingezuilika kama wangefikiwa na huduma za afya kuzuia changamoto
hizo, na huduma hizo siyo huduma ghali kialisia ni huduma za bei nafuu
kabisa lakini hazipo sasa
Ni ukosefu wa haki za kijamii kwa sababu wakati vifo 32 hutoke kila
siku kwa kipindi cha miaka 10, pia ina kadiriwa billion 20 hupotea kila
siku katika bandari ya dar es salaam. Hebu tizama sidhani kamaa kuokowa
vifo hivyo inge gharimu hata milioni 10 kwa siku.
Pia kumekuwapo na mikakati ya kiujumla ya kutatuwa tatizo hili isiyo
zingatia upekee wa maeneo mbali mbali, mfano makete iringa vifo vingi
vya uzazi vilitokana sana na HIV, lakini
Kigoma ni umbali wa huduma za afya..so mikakati lazima iangalie upekee
wa sababu za kimaeneo na siyo kuwa na mikakati ya kiujumla.
Lakini uvunjifu huu mkubwa wa haki za binadamu utaendelea kwa sababu, katika rasimu ya katiba haki ya uzazi Salama haija tajwa.
So hatuta kuwa na sheria, sera, rasilimali za kutu hakikishia uzazi
salama na ulinzi wa mwanamke katika mchakato wa kuleta taifa jipya, .
Je wewe unadhani bila haki ya uzazi salama kuwepo kwenye
rasimu..tutaweza kupata katiba inayolinda na kutetea haki za binadamu??
, kamaa ilivyo bainishwa na umoja wa mataifa????
Kwa nini mwanamke apoteze maisha wakati anapokuwa Ana towa maisha?
Tumpiganie mwanamke wa Tanzania…haki ya uzazi salama itambulike kikatiba
Tuondowe ubaguzi wa jinsia uliotokanaa na wanaume kuwa watunga
sera,sheria, kanuni,maadili…na kukosa jicho la kuangaza ulimwengu wa
wanawake
Happy women’s day
I dedicate this paper kwa mama yangu mpendwa na girl frend wangu….love u guys
My twitter is @nikkwapili na insta ni nikkwapili……karibu kwa maoni yako