Monday, March 3, 2014

YOU HEARD : LORD EYEZ AKUMBWA NA KASHFA NZITO YA WIZI WA LAPTOP


Lord Eyez akiwa chini ya Ulinzi wa Askari
Member wa Kundi la Hip Hop la Weusi mtu mzima Lord Eyez ametajwa na mwanadada mmoja anayedai kuwa ni mume wa Bw. Eli Furaha mfanyakazi wa Vodacom Arusha, amesema eti mume wake ameibiwa na Lord Eyez Laptop aina ya Dell, iliyokua kwenye gari lake lililokua limepaki nje ya Bar moja jijini Arusha, mwanadada huyo amenisimulia eti siku hiyo yeye na mume wake walifika kwenye Bar hiyo kupata Vinywaji na eti Lord Eyez alikuwepo eneo la tukio lakini ghafla wakainuka na kuondoka lakini dakika tano baadae flora na mume wake nao wakawa wanaondoka lakini kufika kwenye maegesho ya magari wakakuta kioo cha gari lao kimepigwa Spray na kuwa chengachenga na Laptop pamoja na hardisk iliyokua pembeni vyote havikuwepo,

Kwa hiyo wao wanamuhisi Lord Na Kundi alilokua nalo siku hiyo, wanandoa hao wakaenda kuripoti polisi msako ukaendeshwa kutoka Ijumaa iliyopita usiku hatimaye alfajiri ya kuamkia siku ya Jumapili Lord Eyez akakamatwa na Jeshi la polisi hadi leo mchana bado msanii huyo alikua anashikiliwa na Polisi, Gazeti la Makorokocho halikuaishia hapo nikacheki na msemaji wa kundi la "Weusi" Nikki wa Pili akatiririka kuwa hana taarifa hizo kwasababu yeye yuko Dar es salaam na tukio hilo linasemekana kutokea Arusha, Bado tunaendelea kufatilia ishu hii, endelea kupiitia Gazeti la Makorokocho online.
Lord Eyez
Hii si mara ya kwanza kwa Lord Eyez kukumbwa na Kashfa nzito awali msanii mwenzake Ommy Dimpoz alimtuhumu Lord Eyez mwaka 2012 kuwa alihusika katika wizi wa vifaa vya gari lake, baadae Dimpoz aka drop kesi hiyo, lakini hapo ni baada ya Lord kukaa katika Selo za polisi kwa muda mrefu.
Msikilize Mwanadada Akifunguka kwenye You Heard ya XXL (Cloudsfm) hapo Chini

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.