Tuesday, April 29, 2014

YOU HEARD : HUYU NDIYE MWANADADA ANAYEDAI KUTEKWA NA NEY WA MITEGO

Grace Sarakikya
Mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Grace Sarakikya amedai kuwa tarehe 14 mwezi huu wa Nne alitekwa na Msanii Bongo flava Ney wa Mitego maeneo ya Kimara, Grace anadai kuwa kabla ya kutekwa alikua anawasiliana na rafiki wa Ney anayeitwa Bonge lakini awali hakujua kama anafahamiana na Ney, sababu ya kuwasiliana na Bonge amesema kuwa Bonge ni camera man na walifahamiana kupitia mtandao wa Instagram na Bonge aliahidi kumpa dili la kuigiza kwenye filamu, wakakubaliana acheze scene 20 kwa malipo ya elfu 50 kila Scene, sasa siku hiyo ya tukio wakapanga kukutana Kimara, Mwanadada Grace akaibuka mpaka kimara akiwa amekodi pikipiki a.k.a Bodaboda lakini kabla ya kufika huko dereva bodaboda alishamtahadharisha kuwa maeneo wanayoenda sio salama, kufika kule akakutana na Bwana Bonge lakini ghafla eti Ney wa Mitego akajitokeza na kumuamuru Bodaboda asepe lakini jamaa alichomoa na kuwaambia lazima aondoke na mteja wake, basi mwanadada akawekwa chini ya Ulinzi na kuamuriwa amuombe msamaha Girlfriend wa Ney anayeitwa Siwema kwa madai kuwa Grace kwa kushirikiana na watu wengine wamekua wakimtukana sana Ney pamoja Siwema kwenye Instagram, mwanadada alikanusha kufanya hivyo na kusema hawajui hao wengine, basi baada ya Grace kumwomba msamaha Siwema kwa njia ya Simu akaruhusiwa na kupewa elfu 15 kama nauli ya kumfikisha kwao, Kwa mujibu wa Grace anadai kuwa Ney alimwambia asisema kokote na yeye aliondoka na hakusema lolote kwa mtu yeyote, Grace akaendelea kudai kuwa ameshangaa siku za karibuni Ney alimpigia na kumtishia amani, Inasemekana Lakini.
Skiza Sauti ya Mwanadada Huyo alipofanya Interview na Gossip Cop Soudy Brown ndani ya You Heard ya XXL/ Cloudsfm

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.