Wednesday, August 6, 2014

YOU HEARD : LINEX AFUNGUKA SIRI YA ZITTO KABWE NA CHAMA CHA SIASA ACT

 
Msanii wa bongo flava Linex Sunday Mjeda hivi karibuni wakati akiongea na Mhariri wa Blog hii ametiririka Siri nzito ya Swahiba wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Mh Zitto Kabwe, siri yenyewe ni kwamba eti mbunge huyo ndiye mwenyekiti wa chama Kipya cha siasa nchini Tanzania kinachoitwa ACT (Alliance for change And Transparency) maana yake ni Umoja wa
Mabadiliko na Uwazi Chama Kipya ambacho kinahisiwa kitakuaja kuwa na nguvu, Linex aliyazungumza hayo wakati anafunguka mipango yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Kasulu Kigoma ndipo nilipomuuliza Je ataingia kwenye siasa kwa tiketi ya Chama gani? Mzee mzima ndo akaanza kufunguka code kuwa yeye ni mwanachama wa ACT na Mwenyekiti wake ni Mh Zitto Kabwe na atamuunga mkono kwa jambo lolote kwa sababu Zitto ni kijana mwenzake.

Mwanzoni mwa mwaka huu wakati taarifa za chama hiki zinatoka jina la Zitto lilitajwa sana kuhusika na chama lakini yeye mwenyewe alikanusha na kudai kuwa yeye ni mwanachama hai wa  "Chadema" inawezekana Mbunge huyu ameweka siri mpaka utakapo karibia uchaguzi mkuu wa Raisi na Wabunge 2015 japo Zitto anakataa kuhusika na ACT Samahani lakini mimi binafsi nashawishiki kuamini kauli ya Linex kwa sababu hizi zifuatazo...
Kwanza Urafiki wa Linex na Zitto Kabwe hauja anza leo, wote wawili ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma, wote wawili ni maarufu na wananguvu katika Jamii lakini pia chini ya Usimamizi wa Zitto mwaka 2012 ulianzishwa muungano wa Wasanii wenye asili ya Mkoa wa Kigoma (Kigoma All Stars) pia ikaanzishwa Kampuni chini ya wasanii hao inaitwa Lekadutigite na walifanikiwa kukusanya maelfu ya wakazi wa Kigoma mwaka Juzi na kupiga bonge la show, hivyo kwa haya yote Linex hawezi kumsingizia Kaka yake,
Msikize Linex wakati akipiga Story na Gossip Cop Tz Soudy Brown wa You Heard ya XXL Clouds fm


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.