Tuesday, September 23, 2014

VIDEO: T.I KU PERFORM SERENGETI FIESTA 2014 (DAR ES SALAAM)

 
Mchana wa Leo kupitia kipindi cha XXL ya Clouds fm Watangazaji B Dozen na Fetty walimtangaza rasmi msanii wa Kimataifa T.I ndiye atakayekuja Nchini Tanzania kwa ajili ya Kutumbuiza kwenye Tamasha kubwa la Burudani nchini maarufu kama Serengeti Fiesta, ambayo imekua ikifanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 13 sasa, na kila mwaka Tamasha hili huwaleta wasanii wakubwa Duniani kuja kutoa burudani kwa watanzania kwa kushirikiana na wasanii wakali wa Bongo Flava, Wasanii wakubwa wa kimataifa waliowahi kuja Tanzania kwenye Fiesta ni pamoja na Shaggy, Ja Rule, 50 Cents, Ricky Rozay,Busta rhymes, Davido, Iyanya, Jay Martins, Koffi Olomide na wengine kibao, Mwaka huu Tamasha hili Dar es salaam litafanyika October 18 na hiyo ni baada ya kumaliza kuzunguka miji 18.
Tazama Video hapo chini ikionyesha Hali ya hewa ilivyokua wakati T.I anatangazwa ndani ya Studio za Clouds fm

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.