|
Rapa Madee Usiku wa leo atashindwa Kulalia Kitanda Chake kama hivi na badala yake atalala kwa kuegamia kuta za selo au kwa kulalia sakafu za selo ambazo mara nyingi zinakua na ubaridi tena hiyo bila shuka bila kuangalia Tv namna hii |
Mpaka mida hii ya saa tano na dakika tatu usiku hakuna Matumaini ya kutolewa selo kwa msanii Madee anayeshikiliwa na jeshi la polisi katika kituo kimoja cha polisi Kigamboni jijini Dar es salaam, Msanii huyu anayewakilisha Kundi la Tip Top Connection inadaiwa na chanzo cha habari hii kuwa siku ya jumamosi iliyopita wakati Madee akiwa pande Vijibweni Kigamboni aliporwa simu yake ya mkononi na vijana wawili waliokua wanaendesha pikipiki moja lakini Madee akiwa na marafiki zake walifanikiwa kuwakimbiza na kumkamata mmoja na mwingine kukimbia na simu hivyo walimchukua yule mmoja ili awatajie alipo lakini mwizi yule aliomba simu awasiliane na ndugu zake baada ya kupewa, katika hali ya kushangaza walikuja Polisi wakiwa na mama wa kijana huyo na kesi akageuziwa Madee na Washkaji zake, hizo ndio taarifa ambazo gazeti la makorokocho imezipata usiku huu.
Mtandao huu unatoa pole kwa Madee kwa kukutwa na matatizo haya.