Thursday, December 18, 2014

DIVA AANDAA TAMASHA LA KUWAKUMBUKA WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI "LIGHTERS UP NIGHT"

Mkurugenzi wa Divas Wild Events Diva Loveness Love jumapili ya tarehe 21 December 2014 ndani ya New Maisha Club Dar es salaam, ameandaa tamasha la kuwa kumbuka watu wote waliotangulia mbele za haki pamoja na kusherehekea maisha yao, akizungumzia na mtandao huu Diva amesema katika miaka ya hivi karibuni kuna Ma Star wengi wametutoka na tulikua tunawapenda sana na kupitia tamasha hili tutawakumbuka kwa pamoja, kwani wana mchango mkubwa kwa jamii hii kwenye nyanja zote siasa michezo uchumi na burudani, watakao sindikiza show hiyo ni Linex, Kamikaze, Peter Msechu, Barnaba, Mirror , Rapper Edu Booy watu maarufu na wasanii wa bongo movie, hii si mara ya kwanza kwa Diva kuandaa tukio kubwa lenye hadhi hii, pia huwa anaandaa Harambee za kuchangia vituo vya watoto yatima.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.