Monday, May 6, 2013

KALAPINA AELEZEA SABABU ZA KUMCHAPA CHIDI BENZ JUKWAANI

Kalapina kulia akiwa na fan wake
Baada ya muasisi wa harakati za hip hop Tanzania Kalapina kumchapa Rapper Chidi Benz katika jukwaa la maisha club alfajiri ya kuamkia leo, Kalapina ameelezea sababu za kutoa dozi hiyo kwa msanii mwenzake, namnukuu " ukweli ni mambo fedheha, mdogo wetu chidi benzi cocaine au heroin / unga anaovuta unampeleka pabaya, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane na matumizi ya madawa kulevya, kwa sababu mwisho wake utakua m'baya, mimi nilikua back stage na ikafika zamu yangu kupanda jukwaani nikawa naskia sauti mtu anatamba jukwaani kwa dakika saba ama nane, alikua ananichelewesha kupanda, na ananiharibia show yangu, huyu mtu si adui, nikatoa amri mara tatu kama F.F.U aka kaidi ndipo nikamfata na kumpa dozi, siku akaanguka chini na mimi nikaendelea na show yangu, hakuna hata mtu mmoja atakaye kubali kuharibiwa kazi, hata rais Kikwete ukimharibia utaishia jela."
source: XXL/ CLOUDSFM

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.