Thursday, January 29, 2015

Polisi Wamkamata Wema Sepetu kwa bajaj eti Adaiwa Kupiga Muziki Kwa Sauti Usiku

Katika hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani linakupa mchapo.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo, Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali, mapaparazi wa GPL walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana (usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti lakini aliwajibu vibaya.
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.

“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama  kwa ajili ya hatua za kisheria,” alisema.
Akizungumza na GPL, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa, alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye sherehe hiyo.
Picha: Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu aliosababisha kwa majirani.Wakachikua spika na kumbeba mwenye sherehe, Neema( rafiki wa Wema Sepetu) kwenye bajaji.GPL

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.