Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.
Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata
mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu
mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.
Habari zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe
katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni
wengine waalikwa.
Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio,
kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati
ya watu wawili.
Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila
ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe
hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani
makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao
hapo.
Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini
alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea
mwenyewe.
"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi
na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr
ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya
kijamii.
Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba
mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu
kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu
yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby
anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na
pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.