Wednesday, January 21, 2015

Ni kutoka kwa Zitto Kabwe kuhusu ishu ya kurudi CHADEMA…

Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa 2014 kulikuwa na story ya mgogoro kati yake na Chama cha CHADEMA.
Magazeti yaliyotoka siku chache zilizopita yaliripoti taarifa ya Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena CHADEMA, millardayo.com imepata exclusive interview na Zitto Kabwe, kazungumzia shu hiyo.
Kuhusu kurudi CHADEMA; “Hapana nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi hiyo haijaamuliwa,bado inaendelea– Zitto Kabwe.
Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa CHADEMA, mtu anaposema nataka kurudi Chadema hayuko sahihi, inafahamika nilikuwa na matatizo na chama hatujaweza kuyatatua, hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo“– Zitto Kabwe.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.