Saturday, January 28, 2017

Mrembo Wa Tanzania Akutana Na Mrembo Wa Kimataifa

Mrembo wa Tanzania Jihan DiMack yupo nchini Ufilipino ambako anaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya warembo wasomi wa vyuo vikuu.


 Moja kati ya vitu ambavyo mrembo huyu anapata nchini humo ni fursa ya kukutana na warembo wengine kutoka mataifa mbalimbali ambao kwa uzoefu wao wanabadilisha mawazo na kupeana mbinu mbalimbali za urembo,


 Zali ambalo Miss Universe Tanzania (Jihan DiMack) amekutana nalo ni kukutana na mrembo wa kimataifa kutoka marekani Ashley Graham.






Ashley Graham ni mrembo mwenye umri wa miaka 28, lakini heshima ambayo anayo mrembo huyo ulimwenguni sio kitu kidogo,



 Ashley amewahi kufanya kazi na Wilhelmina Models, na Ford Models ambao ni mawakala wakubwa wa urembo dunianai.


Ashley pia amewahi kuzipamba kurasa za mbele za majarida kadhaa yakiwemo YM na Harper's Bazaar, GlamourElle  Vogue Magazine.


ANGALIA HII VIDEO YA JIHAN DIMACK NA ASHLEY GRAHAM WALIPOKUTANA: 









Hii ni fursa kwa mrembo wetu Jihan, Huenda uwepo wa Ashley kwenye macho yake ukamuongezea kitu kwenye uelewa wake ambacho moja kwa moja kitamsaidia kusonga mbele zaidi kwenye Career yake.



Watanzania Tunaombwa Kumpigia Kura Kwa wingi kupitia Tovuti ya Miss Universe ambayo ni missuniverse.com



Au kwa watumiaji  wa SmartPhone unaweza Kudownload App Ya Vodi kwa kubofya Hapa.

Imeabaki siku moja tu zoezi la upigaji kura lifungwe,. 




Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.