Mtu mmoja amekatika miguu na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya lori moja kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya Coaster linalofanya safari kati ya Ubungo, Tegeta katika eneo la Tegeta Dar es Salaam.
Taarifa ya kituo cha ITV imesema mafundi gereji wa Tegeta walifanya jitihada kutumia vifaa vyao kukata mabati ya gari ili kuwatoa watu walionasa ndani ya gari iliyokuwa na abiria.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Kamilius Wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu baadaye baada ya uchunguzi kufanyika.