Stage Name: Edu Boy
Tarehe ya Kuzaliwa: 29 June 1993, Bugando Hospital Mwanza
mwaka 2001 alianza Primary School pale Bugando Primary School, Mwaka 2008 hadi 2011 Sekondari alisoma Mwanza Sekondari, wakati akiwa shule alishaanza kushiriki kwa kutoa burudani kwa style ya muziki wa kufoka foka "Hip Hop" kwenye matamasha mbalimbali ya kishule yaliyoandaliwa na kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria "Zinduka" matamasha ya siku ya ukimwi duniani na kwenye Graduation za wanafunzi wenzake,
Mwaka 2013 Edu akashiriki kwenye Tamasha Maarufu linalo andaliwa na Kituo cha Radio kikubwa nchini Tanzania Clouds fm na tamasha hilo linaitwa Serengeti Supa Nyota, tamasha hili hupita katika miji isiyopungua 18 Tanzania bara na Visiwani kwa kutafutwa mwakilishi mmoja kutoka katika kila mji na Edu Boy alifanikiwa kuwa mwakilishi wa mwanza kwa kuwashinda wenzake na kuwa mshindi wa Mwanza, baadae mwaka huo huo Edu Boy akashiriki kwenye fainali za Supa Nyota na kuwa mshindi wa Kwanza kwa kuzoa point nyingi mbele Kiongozi wa Majaji Producer Mkubwa Nchini Tanzania "Lamar" na kuwa "Supa Nyota"
Baada ya mashindano hayo Edu hakulaza damu akarecord ngoma yake ya kwanza inaitwa Scandal kwa kumshirikisha msanii wa RnB Belle 9, Single yake ya pili inaitwa Mwanadamu kwenye chorus amesimama Jux na Vaness Mdee, Single ya tatu ya Edu Boy inaitwa Yes Or No ft Belle 9, ambayo ametoa video yake hivi karibuni chini ya Director Nick Dizo
Sikiliza Mwanadamu by Edu Boy:
Tazama Yes Or No By Edu Boy