WAKATI Cristiano Ronaldo akiangukia kwenye penzi zito la Lucia Villalon baada ya kuachana na Irana Shayk aliyedumu naye kwa miaka mitano, mwanamke huyo naye amejibu mapigo na kuangukia kwenye penzi la staa wa filamu na mieleke , Dwayne Johson "The Rock".
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Marekani, Irina naye ameanza kumsahau Ronaldo na sasa anajiachia na mpenzi wake mpya The Rock ambaye amewahi kuvuma na filamu ya Hercules.
Inasemekana uhusiano wa Irina na bingwa huyo wa WWE ndiyo sababu kubwa ya Ronaldo na mwanamitindo huyo wa Urusi kuachana.
The Rock na Irina wamekuwa wakitokea mara kadhaa wakiwa pamoja kwenye picha ambazo Irina amekuwa akiweka kupitia mtandao wa Instagram.