Kamapuni ya Samsung imetoa wito kwa watu wenye
simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi
kubaini ni kwa nini simu hizo zikiwemo zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa
imethibitisha kwamba ni salama,zinawaka moto.
Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo ulimwenguni.Samsung
iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi
Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba
betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.Lakini sasa taarifa zimetokea kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto baada ya
Mwanamume mmoja jimbo la Kentucky nchini Marekani kudai alikta chumba chake cha kulala kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya Note 7 aliyokuwa ameipata baada ya kurejesha ya awali.
Hata hivyo mapema mwezi huu abiria kwenye ndege moja nchini Marekani walitakiwa kushuka kwa dharura baada ya simu ya Note 7 ya mmoja wa abiria kuanza kutoa moshi kabla ya kuitupa nnje kwa dirishani.
"Kwa sababu usalama wa wateja ni jambo tunalotilia maanani zaidi, Samsung inawataka wasambazaji wote na wauzaji wake kote duniani kusitisha uuzaji na pia ubadilishaji wa simu za Galaxy Note 7 uchunguzi unapoendelea".Ilisema sehemu ya taarifa ya Kampuni hiyo.
Watu wangapi wameathirika;
Samsung inasema simu zilizoathirika ni takriban 2.5 milioni.ambapo kwa mujibu wa kampuni hiyo, simu 45,000 za Note 7 zimeuzwa Ulaya hasa Uingereza huku zaidi ya asilimia 75 ya simu hizo zikirudishwa madukani na wateja ambao walipewa simu nyingine za Note 7 ambazo nazo zimebainika sio salama.
Je Sumsung wamepata hasara;
Kampini ya Samsung kupitia simu hizo za Galaxy Note 7 walitarajia kushindana na kampuni ya Apple iliyoingiza sokoni simu za iPhone 7 lakini baada ya matatizo hayo, Samsung imeathirika baada ya hisa zake kushuka huku hisa za Apple zikizidi kupanda thamani.
-BBC.